September 1, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwanasheria Mkuu :Serikali inaendelea kufanya maboresho Sheria mbalimbali

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Hamza Johari amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya maboresho katika Sheria mbalimbali ili kuweka mazingira wezeshi ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma, wakati akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2026 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2026).

Johari ameeleza kuwa ili kuyafikia malengo ya Dira ya Taifa 2050 ni muhimu mfumo wa Sheria uendelee kuhuishwa ili kuendana na mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kiteknolojia na kimataifa, kuondoa vikwazo vya utekelezaji na kuimarisha mifumo ya usimamizi.

*”Marekebisho ya sheria ni miongoni mwa hatua muhimu za Serikali katika kuweka mazingira wezeshi ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,”amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akiwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2026 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2026) Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametaja Sheria zilizofanyiwa maboresho ni pamoja na Sheria ya Kuzuia Utakatishaji wa Fedha Haramu, Sura ya 423, Sheria ya Nguvu za Atomiki, Sura ya 188, Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania, Sura ya 197, Sheria ya Majina ya Biashara, Sura ya 213, Sheria ya Usafiri wa Anga, Sura ya 80, na Sheria ya Kampuni, Sura ya 212.

Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema pia Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20, Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Sura ya 95, Sheria ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Sura ya 174, Sheria ya Chuo cha Uhasibu Arusha, Sura ya 240, Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1, Sheria ya Usimamizi wa Mahakama, Sura ya 237 na Sheria ya Baraza la Vijana, Sura ya 441.

Vilevile, Johari amesema kuwa Muswada huo unapendekeza kufanya maboresho pia katika Sheria ya Usajili wa Hataza, Sura ya 217, Sheria ya Magereza, Sura ya 58, Sheria ya Usimamizi wa Maabara Binafsi za Afya, Sura ya 136, Sheria ya Huduma za Maktaba Tanzania, Sura ya 102, Sheria ya Bodi ya Utalii Tanzania, Sura ya 364,