August 31, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kiongozi ACT Wazalendo ahimiza uongozi wa hekima

Na Mwandishi wetu,TimesMajira Online,Dodoma

KAIMU Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo Mkoa wa Dodoma Rev David Majanjala amewasihi Viongozi wa ngazi yoyote kuongoza kwa kutumia hekima ili kufanikisha maono waliyonauo.

Rev Majanjala alitoa wito huo mwishoni mwa wiki katika uzinduzi wa vitabu viwili ambavyo vimeandikwa na Dkt.Danieli Mwangili ambavyo ni Uongozi bila kiti na kitabu cha Kinyume cha Mkondo vilivyo zinduliwa Jijini hapa.

Kaimu Mwenyekiti huyo ambaye alimwakilisha kiongozi Mkuu wa Chama hicho Taifa (KC) Dorothy Sem,Rev Majanjala amesema kuwa ili uweze kuwa na uongozi uliotukima ni lazima kutanguliza hekima Kwa kuwa wale unaowaongoza.

Kiongozi huyo amesema kuwa viongozi wengi au jamii kubwa inajikuta katika mafarakano na migogoro kutokana na kukosekana kwa hekima kwa viongozi wanaoongoza au kwa wanaoongozwa.

“Taifa,familia au jamii yoyote inaweza kujikuta ikiangamia au kukosa hekima ya yule anayetawala au anayetawaliwa,na siku zote ili hekima itoweke inasababishwa na roho ya uongozi wa kidikiteta hekima ikikosekana udikiteta utumika ili kuwanyamazisha wanaoongozwa ili wafuate kile ambacho wanaelekezwa hata kama ni kibaya.

“Kiongozi mzuri ni yule anayejitambua ili kufundisha wale walio gizani,uongozi ni taa ya kuwamulikia wengine ili watoke gizani.

Hata hivyo amesema kuwa Watanzania wange wametawaliwa na tabia ya kuishi kwa lalamika na kutengeneza umbea na kushindwa kufikia malengo yanayotakiwa kwa faida yao wenyewe na Taifa kwa ujumla,”ameeleza Rev Majanjala.

Hata hivyo amewataka vijana wenye sifa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika nafasi ya kisiasa wajitokeze kuwanamia nafasi hizo kwani siasa ni hatima inayo ongoza maisha ya kila siku.

Kwa upande wake Mtunzi wa vitabu hivyo Mwangili akielezea kusudi la kutunga vitabu hivyo amesema ni kuhamasisha jamii ya watanzania hususani vijana kujijengea huruka ya kusoma vitabu kwa nia ya kujiongezea maarifa.

Amesema jamii kubwa ya watanzania wana tabia ya kutopenda kusoma vitabu mbalimbali hivyo wanakosa maarifa jambo ambalo linawasananishia kukosa uthubitu wa kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo.

“Nimetunga kitabu cha Uongozi bila Kiti na Kinyume cha Mkondo kwa lengo la kuwafanya hususani kutambua dhana kamili ya uongozi na kuthubutu kufanya mambo makubwa bila kujali mbele kuna kikwazo gani kikubwa.

“Ili uweze kufanikiwa ni lazima kuthubutu na ili uwe kiongozi mzuri ni lazima uwe mwadilifu na hauwezi kuwa mwadilifu kama hauwezi kusoma vitabu mbalimbali ambavyo vinaweza kukupa maarifa na ujasiri wa kusonga mbele kimafanikio,”amesema Mwangili.