
Na Israel Mwaisaka, Sumbawanga
Mkuu wa wilaya ya sumbawanga mkoani Rukwa, Nyakia Ally Chirukile, ameliagiza jeshi la polisi wilaya ya sumbawanga kushirikiana na uongozi wa kijiji cha Malagano, manispaa ya sumbawanga, kufanya msako wa kijana anayedaiwa kumuoa mwanafunzi aliyemaliza elimu ya sekondari na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake jana August 10,2026 alisema kuwa amepata taarifa kuhusu juu ya Mwanafunzi aliyekua anasoma shule ya sekondari Itewele (jina lake limehifadhiwa) ambaye kwa mwaka wa masomo wa 2025 alihitimu masomo ya kidato cha Nne na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule ya sekondari Kizwite Manispaa ya Sumbawanga,akichaguliwa kisoma mchepuo wa HKL
Chirukile alieleza kuwa baada ya kupata taarifa hizo, ameliagiza jeshi la polisi kufanya uchunguzi na kumsaka kijana huyo, ili kuweza kuchukua hatua stahiki za kisheria endapo itathibitika kuwa amekiuka sheria.
aidha, mkuu huyo wa wilaya alisisitiza kuwa serikali haiko tayari kushuhudia watoto wanaochaguliwa kuendelea na elimu wakizuiwa na wazazi au walezi na badala yake kuozeshwa.
alisema atahakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano wilaya ya sumbawanga wanaripoti shuleni na kuanza masomo.
Mkuu huyo wilaya amewataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wa kulinda haki ya mtoto ya kupata elimu na kuacha vitendo vinavyoweza kumkatisha mtoto safari yake ya elimu.
alidai kuwa wazazi watakaobainika kuwaachisha watoto shule na kuwaozesha watachukuliwa hatua za kisheria.

More Stories
Wakulima Kanda ya Kati wavuna na Mixx
Ndejembi awasha umeme Mwanubi Shinyanga
Bima ya mazao kuwa kinga kwa wakulima