Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline
UJUMBE kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) ukiongozwa na Dkt. Crispin Kahesa leo umemtembelea Balozi wa Saratani nchini “Babuu wa Kitaa” kwa lengo la kumjulia hali na kumpa pole baada ya kupata changamoto ya kiafya.
Babuu wa Kitaa alipata maradhi mengine tofauti na saratani akiwa katika shughuli zake za kila siku hali iliyomfanya kufika katika Hospitali ya Rabininsia iliyopo jirani na makazi yake kwa ajili ya kupata huduma za matibabu.
Kwa sasa anaendelea vizuri na hali yake inaendelea kuimarika baada ya kupata huduma ya matibabu.
Ujumbe wa ORCI umeeleza umuhimu wa mshikamano na kuwatia moyo watu wanaopitia changamoto mbalimbali za kiafya huku ikiendelea kushirikiana na jamii katika kutoa elimu ya afya, kinga na umuhimu wa uchunguzi wa mapema wa saratani.


More Stories
Profesa Wabanhu ateuliwa kuwa Makamu Mkuu SAUT
Mradi wa maji wanufaisha wakazi 22,000
Shule 10 kunufaika na mpango wa kuboresha ufaulu