
Na Israel Mwaisaka, Nkasi
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Charles Makongoro Nyerere, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kwa kufanikiwa kupata hati safi , akieleza kuwa mafanikio hayo ni kielelezo cha usimamizi bora wa fedha za umma na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali.
Nyerere ametoa pongezi hizo leo, Julai 14, 2026, wakati akizungumza katika Baraza Maalum la Madiwani la kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Amesema mafanikio hayo yametokana na ufungaji mzuri wa vitabu vya hesabu za Serikali, uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya fedha za umma, usimamizi madhubuti wa rasilimali, ukusanyaji mzuri wa mapato, utekelezaji wa bajeti kwa ufanisi, pamoja na ushirikiano imara kati ya Menejimenti ya Halmashauri na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa mafanikio hayo yanaendelea kuimarisha uwajibikaji, uwazi na usimamizi bora wa rasilimali za umma kwa manufaa ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, huku akiitaka Halmashauri kuendeleza juhudi hizo ili kudumisha viwango vya utendaji na utoaji bora wa huduma kwa wananchi.


More Stories
Kutofahamika kwa taasisi za uwezeshaji kiuchumi nchini chanzo Cha umasikini
Sh.400 mil ,kukarabati makazi ya wazee
PPRA yashinda Tuzo, yaahidi kuendelea kuhudumia wananchi