Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Serikali imesema, Sheria zinapaswa kutumika kama nyenzo ya maendeleo ya taifa kwakuwa ubora wa Sheria hupimwa kwa matokeo yake katika kuboresha maisha ya wananchi, kuvutia uwekezaji, kuimarisha utawala bora na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah alipomuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, katika Uzinduzi wa Kitabu cha Falsafa ya Sheria ya Mama Samia uliofanyika katika Ukumbi wa Maktaba mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),
Aidha, Abdulla, amempongeza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Johari kwa kutoa wazo la kuandikwa kwa Kitabu cha Falsafa ya Sheria ya Mama Samia (Mama Samia Doctrine of Law): Utekelezaji Wake katika Mageuzi ya Kiuchumi na Kijamii.
“Nitoe pongezi za dhati kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Said Johari, kwa kuja na wazo hili muhimu la kuandaa Kitabu hiki,Hamza Johari Nakupongeza sana kwa kazi hii nzuri.” Amesema Abdullah.

Abdullah ameeleza kuwa, Kitabu hicho kilichoandaliwa kwa uratibu wa Chama cha Mawakili wa Serikali, kimebeba maudhui mengi ambayo yamefanyika chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ikiwemo mageuzi na maboresho makubwa katika Sekta ya Sheria.
Vilevile Makamu wa Pili wa Rais ametumia nafasi hiyo kuwahimiza Watanzania kuendelea kudumisha amani na mshikamano nchini, kwani bila amani hakuna maendeleo na uchumi endelevu.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Zainab Katimba amempongeza Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mlezi wa Chama cha Mawakili wa Sarikali Tanzania, (TPBA) Mhe. Hamza Johari, kwa kuzindua Kitabu hicho kwani kitasaidia kuboresha masuala mbalimbali katika Sekta ya Sheria.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali, Wakili Bavoo Junus amesema,wazo la kuandika kitabu hicho lilizaliwa Juni 21, 2025 wakati wa Kongamano la Kitaifa la Kisheria baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Hamza Johari kupendekeza kuandaliwa kwa andiko litakalochambua nafasi ya sheria.


More Stories
SMAUJATA waipongeza HGWT kupambana na Ukatili Mara
FCC yajipanga kuendelea kulinda ushindani maslahi ya walaji
Tutuba ahimiza matumizi ya Taasisi rasmi za fedha