Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
UZALISHAJI wa zao la Mkonge umeongezeka kutoka tani 30,000 mpaka tani 40,000 kwa mwaka hadi kufikia tani 72,000 kwa mwaka.
Hayo yameelezwa leo Julai 2,2026 na Ofisa Masoko wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Besti Lutanda alipotembelewa na TimesMajira online kwenye Banda la Mkonge lililopo katika Maonesha ya 50 ya kimataifa ya biashara jijini Dar es Salaam.

Lutanda amesema kwa miaka mitano iliyopita uzalishaji wa mkonge na mazao yake ulikuwa kati ya tani 30,000 hadi tani 40,000 kwa mwaka hali iliyozorotesha ustawi wake.
“Mafanikio ya bodi ya Mmkonge yanaonekana kwa vitendo hivi sasa uzalishaji umeongezeka hadi kufikia tani 72,000 kwa mwaka huku mahitaji ni zaidi ya tani 100,000 kwa mwaka.

“…Ndio maana sisi bodi ya mkonge tunajivunia uwepo wa miaka 50 ya maonesho haya ya kimataifa ya biashara yanashirikisha wawekezaji kutoka kila pembe ya dunia,” amesema Lutanda.
Ameongeza kwamba licha ya kusafirisha na kuuza malighafi za mkonge ndani na nje ya nchi, vijana wa Tanzania wanaongeza thamani ya zao hilo kwa kutengeneza mabegi na vitu mbalimbali vinavyotokana na zao hilo.

Ofisa masoko huyo alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania kulima zaidi mkonge kwa kuwa thamani yake ni kubwa kwa muda mrefu.
Alisema thamani ya tani moja ya singa za mkonge ni kati ya sh. Mil. 2.2 mpaka sh. Mil. 4.2 kulingana na daraja na ubora wake.

More Stories
Waziri Kapinga apongeza mafanikio ya TTCL
Makinda apongeza jitihada za Serikali kuhamasisha Nishati Safi ya Kupikia
TTCL yaendelea kuwekeza katika vitendea kazi