
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mwigulu Mchemba ameunga Mkono juhudi zinazofanywa na Mbunge wa Mbeya mjini Patrick Mwalunenge kuwataka wajasiliamali wadogo wajiunge na vikundi vya SACCOS ili wasajiliwe.
Waziri Nchemba ameyasema hayo kwa njia ya simu wakati wa Mkutano baina ya wafanyabiashara wadogo na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini na Viongozi wandamizi Mkoani humo.
Akizungumza kwa njia ya Simu kwenye Mkutano huo Waziri Mkuu Nchemba amesema kuwa iwapo kikundi chopchote kitaanzisha umoja wao kupitia SACCOS zao yeye atakuwa tayari kuchangia kiasi cha Shillingi Million 20 kwa kila kikundi.
Amesema jambo la Msingi ni kuanzisha vikundi kisha kuvisajiri ili waweze kuwezeshwa na kupata usimamizi mzuri kwa lengo la kujiendesha pasipo kuwa na malumbano au usimamizi mbovu.
Mbunge wa Mbeya Mjini Patrick Mwalunenge amekuwa akiendesha mafunzo kwa wajasiliamali wadogo kwa lengo la kuwapatia elimu ya kujiendesha wenyewe kwa lengo la kuondokana na mifumo kandamizi ya liba.
Mbunge huyo amesema vijana wakiwemo Bodaboda, Mafundi cherehani, Mama Ntilie, na makundi mengine waanzishe SACCOS zao ili wazisajili na kuanza kuchangishana kiasi kidogo kama elfu Moja kama kianzio chao jambalo linaweza kuwainua kipato chao.
Awali kumekuwepo na upotoshaji Mkubwa kwa baadhi ya wanasiasa ambapo wamekuwa wakieneza taarifa potofu wakidai kuwa Mbunge huyo amewataka Bodaboda kuchangia 1000 kwa lengo la kujenga barabara j ambalo amesema sio kweli.
Amesema kuwa Mkoani humo kuna baadhi ya vikundi ambavyo vilianzishwa kama vile Iwamu SACCOS ambayo ilianzishwa na wakulima lakini kwa sasa inafanya kazi kama Benki.

Amesema kutokana na uingi wa waendesha Bodaboda Mkoani humo pamoja na Mama lishee, mafundi cherehani wanaweza kuanzisha kikundi kikubwa sana ambapo fedha wanazoweza kupata kwa mwezi inaweza ikazidi hata Billion mbili.
“Nasikitika sana kutokana na taarifa za upotoshaji kuhusu kauli yangu niliyoitoa Bungeni na watu wakanukuu kifungu kidogo ambacho mimi niliitolea mfano” anasema Mwalunenge.
Mwalunenge amesema kabla hajawasilisha hotuba yake Bungeni tayari alikwishakaa na wajasiliamali na kuwaeleza lengo lake la kuanzisha SACCOS ili aweze kuwasaidia pamoja na kuwa na mifumo inayoweza kuwarahisishia kupata mikopo kwenye taasisi za kibenki.
Wakati Mwalunenge akiyasema hayo nae Mchungaji na Nabii wa Kanisa la Tample of prayer for all nations Nabii Charles Mkuvasa ametoa wito kwa watanzania kulinda amani na kuwa wazalendo wa taifa lao hasa kipindi hiki ambapo taifa linahitaji maridhiano ya kitaifa.
Mkuvasa ameyasema hayo jana wakati akiongea na Chombo kimoja cha Habari Wilayani Kyela Mkoa wa Mbeya nakutoa wito kwa watanzania hasa vijana kuwa wazalendo na kulinda amani iliyoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambalage Nyerere.
Mchungaji huyo amesema Tanzania ni moja ya Nchi iliyobarikiwa hapa duniani kutokana na uwepo wa Njia kuu Tatu kutoka kwa Mungu.
Amesema Tanzania ni Taifa lenye milango mitatu afrika mashariki na kati ya kuingilia kama ambavyo historia inavyosema taangu wakati wa Wakoloni.
Nabii huyo amesema Mlango wa kwanza kwa Tanzania ni ule ambao wakoloni walipitisha watumwa kwenda Uarabuni na Ulaya na Mlango wa Pili ni Ukombozi wa Afrika.
Amesema katika kukomboa mataifa ya Africa Mwalimu Nyerere ndiye alikuwa kinara wa kusuka mipango kwa viongozi waliotaka mageuzi kwa mataifa yao hasa mataifa jirani ili watoke katika dhana ya utumwa.
Amesema kuwa Mwalimu alikuwa kama Musa kuokoa wa Afrika na kudai kuwa huu ni wakati wa Tanzania wa sasa ambao ni pamoja na vijana kulikomboa Taifa lisiingie katika nguvu za giza.
Aidha amesema kuwa lango la Mwisho ni Umoja wa Taifa ambapo amesema Mungu alimpa Maono Rais wa Kwanza Hayati Mwalimu Nyerere ya kukusanya makabila yote kuwa watu wamoja na kutumia lugha moja ili kulinda amani ya Nchi.
“Kwa njia hii Mungu akampa Mwalimu hekima kubwa ili kuleta amani kwa taifa letu lakini kwa sasa amani hiyo tumeanza kuichezea na kusahau yale maono ya Baba wa Taifa aliyopewa na Mungu, ni hatari saana” anasema Nabii Mkuvasa.
Mkuvasa ameongeza kuwa hata kauli aliyoitoa Mbunge wa Mbeya Mjini Patrick Mwalunenge haikuwa na madhara bali inamaono makubwa kwa vijana wasio na ajira rasmi lakini kutokana na siasa za kutokuwa na uzalendo wakaibadili kauli ile na kuipotosha kwa jamii.
“Yule Mbunge ukiifuatilia hotuba yake ndipo utagundua kuwa ile hotuba inakwenda kuwakomboa vijana kutoka kwa wanyonyaji hasa kwa waendesha Bodaboda na makundi mengine lakini sasa watu wamekwenda kuibadili ili ionekane kama haina tija kwao”
Mkuvasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Simama na Mama.Ametoa wito kwa vijana kuacha kushabikia na kufuata mikumbo ambayo haina tija kwa bali wasikiliza na kuheshimu utaifa wao ili amani iweze kudumisha kwa kumuenzi baba wa Taifa.
Awali baadhi wa wanasiasa walinukuu vibaya kauli au hotuba ya Mbunge huyo na kuipotosha kwa kusema kwamba wafanyabiashara wadogo wadogo watalazimika kuchangia fedha kwa lengo la Serikali kujengea barabara jambo ambalo sio kweli.
Aidha amesema kuwa kama Mbunge ataendelea kutoa elimu kwa vijana walio kwenye makundi mbali mbali ili waweze kuondokana na fikra potofu wanazolishwa na baadhi ya wanasiasa ili waweze kujitambua namna ya kujiinua kiuchumu.

More Stories
Mlipuko wa baruti wasababisha kifo,majeruhi saba
Mahundi:Malezi Bora uwekezaji maendeleo ya Taifa
NMB yaanza rasmi huduma za kibenki SabaSaba