Na Mwandish wetu,Timesmajimra
Wakazi na wageni wa Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (DITF) sasa wameanza kupata huduma za kibenki ndani ya Viwanja vya Saba Saba kupitia Tawi la NMB Saba Saba, linalofanya kazi kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2026.
Tawi hilo linatoa huduma za kufungua akaunti, kuweka na kutoa fedha, malipo ya Serikali, bima na huduma za kidijitali, pamoja na ATM na mawakala waliopo viwanjani.

Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, William Nkuna, ameseema tawi hilo linalenga kusogeza huduma karibu na wananchi na wafanyabiashara wanaohudhuria maonesho.
Pia, NMB inatoa ushauri wa mikopo na huduma za kidijitali, huku wateja wakipata mikopo ya hadi Sh milioni 2 na wafanyabiashara hadi Sh milioni 5 kupitia simu.

More Stories
Mahundi:Malezi Bora uwekezaji maendeleo ya Taifa
Waziri Mkuu aunga mkono hoja ya mbunge wa Mbeya mjini juu ya Bodaboda kujiunga kwenye vikundi
Rais Chapo kufungua rasmi maonesho ya Sabasaba 2026