September 30, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Habib Kondo aelezea vipigo kwa timu yake

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online.

KOCHA Mkuu wa timu ya Manispaa ya Kinondoni KMC FC, Habib Kondo amesema bado ana imani na kikosi chake licha ya kupoteza mechi mbili za Ligi Kuu msimu huu.

Kondo ametoa kauli hiyo leo wakati KMC FC, ilipokuwa ikifanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa mzunguko wa sita dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Oktoba 14 mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Amesema kupitia mazoezi hayo, timu hiyo inajiandaa kikamilifu katika kujiweka vyema dhidi ya mchezo huo na kwamba makosa yaliyofanywa na wachezaji wake katika mchezo uliopita yanafanyiwa kazi.

Habibu amesema anakiamini kikosi chake kwa kuwa kinauwezo mzuri, ila kikubwa kwa sasa ni kuendelea kujenga utulivu kwenye safu ya ushambuliaji ili kupata matokeo mazuri katika mchezo huo.

“Timu inatengeneza nafasi nzuri za kufunga lakini kwenye umaliziaji inakuwa changamoto, kupitia mazoezi haya, tunakwenda kukisuka kikosi chetu ili kwenye michezo ijayo tupate matokeo ambayo awali tulikuwa tukiyapata,” amesema.