Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Wanahisa wa NMB Bank PLC wameidhinisha mgawanyo wa hisa kwa uwiano wa hisa 10 kwa kila hisa moja, hatua inayolenga kufanya hisa za benki hiyo ziwe nafuu zaidi na kuongeza ushiriki wa wananchi katika umiliki kupitia soko la mitaji.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NMB Bank PLC, David Nchimbi, amesema hatua hiyo inalenga kupanua umiliki na kuongeza ushiriki wa wananchi katika soko la mitaji, hasa baada ya hisa za NMB kuwa ghali zaidi miongoni mwa hisa za benki zilizoorodheshwa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Bank PLC, Ruth Zaipuna, amesema mgawanyo huo umefika wakati muafaka kwa kuwa unalenga kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kushiriki katika kujenga utajiri kupitia umiliki wa hisa. Utekelezaji wake utategemea vibali vya mamlaka husika.

Mkutano huo wa 26 wa Mwaka pia uliidhinisha gawio la rekodi la Sh bilioni 305, sawa na Sh 610.15 kwa kila hisa, likiwa ni gawio kubwa zaidi kuwahi kutolewa na taasisi ya fedha nchini. Gawio hilo limechagizwa na matokeo imara ya mwaka 2025, ikiwemo faida kabla ya kodi ya Sh trilioni 1.1 na faida baada ya kodi ya Sh bilioni 756.




More Stories
REA yazindua usamabazaji majiko banifu Songwe
Mapato ya Ndani yaimarisha Bajeti ya Serikali
Salome:Ushirikiano wa wadau ni muhimu kufikia lengo la Nishati Safi ya Kupikia