Na Mwandishi wetu,Timesmajira
KAMPUNI ya Kitanzania ya Ngoteya Wild, inayoongozwa na muandaaji wa makala zenye maudhui ya uhifadhi na wanyamapori Hans_Cosmas_Ngoteya, imetangaza kuzindua filamu yao mpya ya Sentinels of Engaruka mnamo Juni 21.
mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habar leo jijini Dar es salaam na Kampuni hiyo imesema filamu imefanya kwa kushirikiana na African people and wildlife ambayo itaoneshwa rasmi kupitia YouTube channel yao .
Imesema filamu hiyo imechukua zaidi ya miaka mitatu kuandaliwa, ikihusisha utafiti wa kina, upigaji picha wa mazingira ya asili na simulizi inayoonesha uhusiano wa kipekee kati ya jamii ya Kimasai, twiga na mazingira ya Engaruka mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa Hans Ngoteya, filamu hiyo inalenga kuhamasisha uhifadhi wa maliasili, kuonesha utajiri wa urithi wa Tanzania na kuifikisha hadithi ya Engaruka kwa hadhira ya kimataifa kupitia jukwaa la YouTube.
Sentinels of Engaruka ni moja ya miradi mikubwa ya filamu za uhifadhi iliyotayarishwa nchini Tanzania, ikiwa na lengo la kuonesha namna jamii na wanyamapori wanavyoweza kuishi kwa maelewano huku wakilinda mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.




More Stories
REA yazindua usamabazaji majiko banifu Songwe
Mapato ya Ndani yaimarisha Bajeti ya Serikali
Salome:Ushirikiano wa wadau ni muhimu kufikia lengo la Nishati Safi ya Kupikia