Na Mwandishi wetu,Timesmajira
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Mazimgira Duniani yatakayofanyika jijini Dodoma Juni 5 mwaka huu.
Katika hafla hiyo, kunatarajia kufanyika kwa uzinduzi wa Programu ya mageuzi ya kimkakati ya Mazingira endelevu Tanzania (2026 – 2030).
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Masauni, amesema kwamba uzinduzi wa Programu hiyo ni nyenzo ya kuwezesha utekelezaji wa Dira ya 2050 na zaidi inayohusu hifadhi ya mazingira na ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Pia Waziri Masauni, ametoa wito kwa wakuu wa mikoa yote Tanzania Bara na Mamlaka za Serikali za Mitaa kushiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo kwa namna ambavyo wamejipanga kwa kushirikiana na wadau kwa kutumia radio za jamii kwa lengo la kuielimisha jamii kuhusu masuala ya hifadhi ya mazingira ikiwemo kutumia nishati mbadala na njia sahihi za kuhifahi taka.
Awali, Masauni amesema kwamba katika kuadhimisha maadhimisho kuanzia leo Mei 11, 2026 shughuli kadhaa zitafanyika kuelekea kilele ni utoaji elimu Kwa umma kuhusu masuala ya uhifadhi mazingira na mabadiliko ya tabianchi.
Pia viongozi na wananchi watashiriki katika zoezi la upandaji miti na kufanya usafi wa mazingira katika majiji ya Dodoma, Tanga, Arusha, Mwanza na Dar es Salaam.
Aidha Mei 15, 2026 kutakuwa na shughuli ya upandaji wa miti katika eneo la Bwawa la Kidete, wilayani Kilosa mkoani Morogoro na Mei 26, kutakuwa na Kongamano la Vijana linalohusu Hifadhi za Mazingira litakalifanyika katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa Mei 28, kutakuwa na Kongamano la Kisayansi na Utafiti wa Mazingira ambayo ni mojawapo ya shughuli za maadhimisho ya miaka 40 ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na uzinduzi wa Kongamano la Wadau wa Mazingira litakalofanyika katika ukumbi JNICC Dar es Salaam litakalohusisha washiriki wapatao 1000 kutoka Afrika Mashariki na jirani.
Waziri Masauni pia amesema Juni Mosi hadi 5 kutakuwa na maonesho ya teknolojia na ubunifu kuhusu shughuli za uhifadhi wa Mazingira yatakayojumuisha wadau kutoka Wizara, taasisi, mashirika ya umma, taasisi binafsi, asasi za kiraia, Vijana na makundi mbalimbali na yatafanyika katika viunga vya Kituo cha mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma ambako kutakuwa na mabanda 100.


More Stories
Ruth Zaipuna kuipeleka NMB Jukwaa la Kimataifa Cambridge
TPDC yaongoza uchimbaji wa Gesi Songo Songo
Tanzania yahimiza mageuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa