April 29, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamati kuu CCM yampitisha Mtafikolo kugombea ubunge Isimani

Na Mwandishi wetu,Dar

Chama cha Mapinduzi (CCM), kupitia
Kamati Kuu, kimemteua, Emmanuela Mtafikolo, kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Isimani, lililoko Wilaya ya Iringa Vijijini.

Taarifa hiyo imetolewaAprili 29, 2026 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo Kenani Kihongosi.

Uchaguzi huo unafanyika ili kujaza nafasi iliyoacha wazi baada ya aliyekuwa mbunge katika jimbo hilo William Lukuvi kufariki dunia.