November 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TBS yatoa mafunzo kwa wadau
wa mafuta zaidi ya 1,700

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetekeleza mpango wa mafunzo kwa wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa mafuta ya kula zaidi ya 1,700 kwa kuwaelimisha kuhusu uzalishaji bora, uhifadhi sahihi wa bidhaa za mafuta hasa sehemu za kuuzia, ufungashaji sahihi na salama na umuhimu wa kuzingatia na kuweka taarifa sahihi na muhimu kwenye vifungashio.

Mafunzo hayo yametolewa na shirika hilo kwa wadau hao wa Kanda ya Kati kuanzia Septemba 21, mwaka huu hadi Oktoba 1 katika maeneo ya Mkalama, Kiomboi, Sikonge, Urambo, Shelui, Manispaa ya Tabora,Nzega.

Maeneo mengine ni Igunga, Manispaa ya Singida, Kondoa Irangi, Kongwa, Mpwapwa, Kibaigwa, Chamwino, Itigi, Manyoni, Dodoma jiji na Bahi.

TBS imetoa mafunzo hayo kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara, Shirika la Viwanda Vigogo Vigogo (SIDO), maOfisa biashara, afya na maendeleo wa wilaya.

Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS, Lazaro Msasalaga, amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajulisha wadau wa mafuta ya kula fursa zilizopo ndani ya Serikali ili kuwawezesha kuboresha bidhaa zao ili ziweze kukidhi matakwa ya viwango na hatimaye kupananua wigo wa soko la ndani na nje ya nchi na kuwafanya kuongeza uzalishaji utakaopelekea kuinua uchumi wao.