Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MIXX by Yas imezindua Wakala App, jukwaa la kisasa na la kwanza sokoni, linalolenga kubadili namna mawakala wanavyoendesha biashara zao na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa zaidi ya wateja wake milioni 22 kote nchini.
Uzinduzi huo ulifanyika Machi 27, 2026, wakati wa hafla ya Partners Gala umefanyika Mlimani City, ambao umewakutanisha mawakala wake wakuu wote, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea mafanikio ya mwaka uliopita na kufungua dira mpya ya mwaka huu.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Angelica Pesha, amewashukuru mawakala na kusisitiza nafasi yao muhimu katika mafanikio ya kampuni hiyo

“Ninyi ndio mnaowafikia wateja wetu kila kona ya nchi, na kupitia juhudi zenu, nidhamu yenu, na ubora wa huduma mnazotoa, mmejenga msingi imara wa mafanikio ya Mixx.
“Mafanikio haya yamejengwa juu ya uwazi, uaminifu, na huduma bora kwa wateja wetu, na ndiyo maana Mixx imethibitishwa na GSMA Mobile Money, ikithibitisha kuwa mifumo yetu inakidhi viwango vya juu vya kimataifa vya usalama, uwazi, na ulinzi wa taarifa za wateja.” Amesema Pesha
.
Akielezea kuhusu ubunifu huo mpya, Pesha amesema:
“Wakala App ni suluhisho ya kwanza sokoni inayowapa mawakala uwezo wa kusimamia biashara zao kwa ufanisi zaidi, kufuatilia utendaji kwa urahisi, na kuwa na udhibiti kamili wa shughuli zao za kila siku.
“Hii inaendana na dira yetu ya kujenga mfumo wa wakala wa kidijitali, wenye ufanisi na unaoweza kukua kwa kiwango cha juu.

”Sambamba na uzinduzi wa Wakala App, Mixx pia imeanzisha huduma ya mikopo kwa Mawakala wakuu inayowawezesha kupata mtaji wa kufanya kazi ili kukuza biashara zao na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa,” amesema.
Kupitia hatua hizi, Mixx inaendelea kuimarisha nafasi yake kama kiongozi wa ubunifu katika huduma za kifedha, kwa kuweka mkazo katika uwezeshaji wa mawakala, ufanisi wa huduma, na upatikanaji wa suluhisho za kisasa kwa Watanzania.
“Safari yetu ya mwaka huu ni ya ukuaji, ubunifu, na mafanikio ya pamoja. Tunaenda mbele tukiwa na zana bora zaidi, uwezo mkubwa zaidi, na maono makubwa zaidi ya mafanikio,” ameongeza Pesha.
Kwa kuwekeza katika teknolojia na uwezeshaji wa mawakala, Mixx inaendelea kujenga mfumo imara unaochochea ujumuishaji wa kifedha na maendeleo ya uchumi nchini Tanzania.

More Stories
NMB ilivyosaidia Serikali kukusanya zaidi ya Sh trilioni 9.8
Serikali yaongeza nguvu kwa wachimbaji wadogo,yasisitiza usalama Migodini
REA imeleta mageuzi sekta ya nishati