January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bil 5.26/- zatumika kujenga barabara Ngara

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online. Ngara

SHILINGI bilioni 5.26, zimetolewa kupitia Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara katika Wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

“Kati ya hizo, sh. bilioni 1.1 zimetengeneza barabara kwa kiwango cha lami kilomita 4.5 katika makao makuu ya wilaya hii.”

Hayo yamesemwa jana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Rulenge, katika mikutano uliofanyika kwenye stendi ya Rulenge.

Amesema kiasi kingine cha sh. bilioni 4.16, zimetolewa kupitia TARURA kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara ikiwemo Muhweza–Mukarehe, Keza–Nyanzovu, Mukalinzi–Mulonzi, Kibuba–Gwenzaza, Murugwanza-Runzenze (Airstrip), Chivu-Ntobeye–Nyakiziba, Buhororo– Mukididili, Ngara – Kumutana na Buhororo-Ruganzo (Airstrip).