March 20, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamba,Kanza washiriki mkutano wa Powering African Summit

Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Else Sia Kanza wameshiriki katika ufunguzi wa awali wa Powering African Summit Machi 19, 2026 jijini Washington Dc.

Mkutano huu wa siku mbili unawakutanisha viongozi wa Serikali, wawekezaji na wadau wa sekta ya nishati kujadili mustakabali wa nishati barani Afrika, fursa za uwekezaji, pamoja na suluhisho endelevu kwa maendeleo ya sekta hiyo.

Katika mkutano huo, Naibu Waziri ameambatana na wataalam kutoka TANESCO, PURA pamoja na REA ambao watashiriki kwenye majadiliano kuhusu upatikanaji wa umeme kwa wote, uwekezaji katika ‘Energy Mix’ pamoja na usimamizi na maendeleo endelevu ya rasilimali za gesi na mafuta.