Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Bukombe
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wameonesha kuridhishwa na kushangazwa na kasi ya teknolojia inayotumika katika kituo cha mfano cha uchenjuaji dhahabu cha Katente, kilichopo wilaya ya Bukombe, mkoani Geita.
Hayo yamebainishwa Machi 15,2026 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini,Subira Mgalu, wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya kituo cha mfano cha Katente kilichoanzishwa na Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Ambapo lengo la kuanzishwa kituo hicho ni kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini katika uchenjuaji bora ili kuachana na matumizi ya kemikali hatarishi kama zebaki.
Mgalu ameeleza kuwa , kamati imefurahishwa na teknolojia hiyo ya uchenjuaji inayotumia mifumo ya kisasa ya Vat Leaching,ambayo imefanikiwa kuongeza kiwango cha upatikanaji wa dhahabu kutoka asilimia 40 hadi kufikia zaidi ya asilimia 90.
Pia, ameipongeza STAMICO kwa kurahisisha upatikanaji wa kemikali , na vilipuzi huduma nyingine zinazoendana na uchimbaji mdogo kwa wachimbaji wadogo wapatao 1019 kupitia kituo cha mfano.
Sambamba na hapo, Mgalu ameipongeza Serikali kwa kusogeza huduma kwa wachimbaji wadogo kupitia kituo cha Katente, hatua hii inawasaidia
wachimbaji wadogo katika kuongeza tija kwenye shughuli zao za uchimbaji.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameishukuru Kamati ya Bunge kwa ushauri mzuri kuhusu kuboresha kituo cha mfano ili kuendana na idadi ya wachimbaji wadogo katika kuwapatia huduma.

Awali , akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za uchenjuaji katika kituo cha mfano cha Katente, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO,Deusdedith Magala,amesema kuanzia mwaka 2020 hadi Januari 2026,wachimbaji wadogo 1920 wamepata elimu juu uchimbaji , usagaji mbale, uchenjuaji na ukamatishaji dhahabu.



More Stories
JAI yapanga kulisha wagonjwa zaidi ya 1,800 Eid El-Fitr, yafanya hafla ya uchangishaji
Sema na Waziri kutatua changamoto za kisheria kwa wananchi
Rais Zanzibar aipongeza Yas, Mixx mageuzi ya kidigitali