
Na Israel Mwaisaka Rukwa
Wanawake wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) Mkoa wa Rukwa wamethibitisha kuwa wataelekea Musoma, Kanda ya Serengeti Machi 7 kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, wakisisitiza kuwa maandalizi yote yamekamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kushiriki Misa maalum katika Parokia ya familia takatifu Kizwite, Mwenyekiti wa BAWACHA Mkoa wa Rukwa, Aida Khenani, amesema safari hiyo haiwezi kuzuiwa kwani kukutanika kwa wanawake kujadili masuala yao si kosa kisheria.
Aida amesema kama kuna changamoto ya kisheria kuhusu mkusanyiko huo, ni wajibu wa Mahakama kutoa tamko kabla ya Machi 8, huku akisisitiza kuwa hawapingani na vyombo vya sheria na wanaheshimu misingi ya utawala wa sheria.
Ameeleza kuwa Siku ya Wanawake Duniani ni maadhimisho ya kimataifa na si mali ya chama chochote cha siasa, hivyo zuio lolote lisilenge kundi maalum la wanawake.
“Mwanamke ni mwanamke bila kujali chama, dini au itikadi,” amesema.
Aidha, ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kupitia upya maamuzi yoyote yaliyotolewa kuhusu mkusanyiko huo, akisema si jambo baya kurekebisha maamuzi yenye utata, hasa katika taifa linaloongozwa na mwanamke

More Stories
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama
Kihongosi amtaka mkandarasi kuwalipa vibarua stahiki zao