
Na Israel Mwaisaka, Rukwa
UMOJA wa mafundi mkoa Rukwa kupitia Magic Builders Foundation umepata viongozi wapya watakaouongoza umoja huo kwa kipindi Cha miaka mitatu ijayo.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Libori mjini Sumbawanga Jana March Mosi 2026,Mwenyekiti wa uchaguzi Evarist Futakamba Mohammed alimtangaza Moses Simtowe kuwa Mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti ,Makamo Mwenyekiti Jerry Mwaijwanga, Katibu Mkuu Avary Gregory.
Wengine ni Katibu msaidizi Shambani Nyangindu,Katibu mkuu,Mtunza hazina Jabir Sanga, Mwenyekiti wa nidhamu Linus Kalikwenda na Musa Mzapora alichaguliwa kuwa Afisa habari.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti Moses Simtowe aliwataka mafundi kuwa wamoja na kushirikiana kwa Kila jambo lakini kubwa ni kuhakikisha mafundi wanakua na mikataba halisi ya kikazi na wateja wao ili kuondoa changamoto za kulaumiana kati Yao na wateja wao na kutengeneza uhasama
Alidai kuwa umoja huo ukiimarishwa una nafasi hata ya kuomba kazi serikalini kupitia mfumo wa Nest na kuzifanya kazi hizo kwa uhuru badala ya kuendelea kuajiliwa na Wakandarasi wanaoshika kazi hizo na mwisho wa siku wanaishia kunyonywa na matajiri hao na kukosa mtetezi na kuwa Sasa mtetezi amepatikana ambaye ni umoja huo.
Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Frank Lupimo kwa upande wake aliupongeza umoja huo kwa kufanya uchaguzi mzuri na wenye uwazi na kuwa wao kama viongozi wa Serikali wanathamini hicho kilichofanyika na kuwa wapo tayari kushirikiana nao katika changamoto zao hasa zinazogusa masalahi yao.
Alisema kuwa ni muhimu kwao Sasa baada ya kutengeneza umoja tena wenye nguvu kupigania haki zao na wao wapo tayari kuwasaidia na kuwashauri wenzao kuwa waaminifu katika kazi zao ili kazi Yao iweze kuwaletea mafanikio.

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina