
Na Israel Mwaisaka, Nkasi
Halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imeanzisha kampeni ya kutokomeza milipuko ya magonjwa ikiwemo kipindupindu na homa za matumbo kwa kuhamasisha jamii kufanya usafi wa mzingira kwenye maeneo ya biashara na makazi.
Mkuu wa wilaya hiyo Peter Lijualikali kupitia kampeni ya usafi iliofanyika katika uwanja wa Saba saba wilayani humo, amebainisha kuwa zozezi hilo litakuwa endelevu na kwamba litakuwa likifanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi na kubainisha kuwa lengo ni kutokomeza milipuko ya magonjwa ikiwemo kipindupindu, kuhara damu, homa ya matumbo (typhoid), na maambukizi ya minyoo.
Kwa upande wake mkuu wa Kitengo cha Usafi na usimamizi wa taka ngumu wilayani humo Mayuma Nzilatuzi, amesema licha ya hilo kampeni hiyo inalenga kuhamasisha jamii kufanya usafi nyumba kwa nyumba ikiwemo kufukia madimbwi ambayo yanaweza kuwa chanzo cha mazalia ya Mbu.
Baadhi ya wananchi wameipongeza serikali kwa kuanzisha kampeni hiyo na kuomba zoezi hilo kuenda sambamba na uhamasishaji wananchi kujenga vyoo bora

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina