
Na Israel Mwaisaka,
Nkasi Mbunge wa jimbo la Nkasi kusini Moses Kaegele amesikitishwa na utekelezaji mbovu juu ya mradI wa ujenzi wa Kituo Cha afya Cha Kate baada ya vifaa vya ujenzi kukaa muda mrefu na kuharibika.
Akizungumza baada ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Kituo Cha afya Cha Kate Kaegele ameonyesha kutoridhishwa na Kasi ndogo ya utekelezaji wa mradi huo wakati Serikali kwa upande wake ilishatoa Mil.500.
Amesema kitendo cha kuacha vifaa viharibike kwa sababu ya kusimama kwa mradi huo ni uharibifu wa mali za Serikali na kutowatendea haki Wananchi ambao wanasubiri huduma katika Kituo hicho Cha afya .
Hivyo amewaomba watekelezaji wa mradi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa,huku akimshukuru Mhe,Rais kwa namna anavyotoa Fedha za maendeleo kwa lengo la kusogeza huduma stahiki za Wananchi.
Mbunge Kaegele pia amedai kuwa Ile ahadi ya barabara ya Nkundi-Mkangale kuitoa TARURA na kuipelekea TANROAD umefanikiwa na hivyo kuwa na uhakika wa barabara hiyo kuwa bora na kupitika wakati wote na kuwa barabara hiyo ni muhimu sana kiuchumi na yenye manufaa makubwa kwa kwao.

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina