Na Zena Mohamed,TimesmajiraOnline,Bahi.
DIWANI wa kata ya chali Wilaya ya Bahi, Pius Mwaluko amewaagiza Kamati ya Mazingira Chikopelo na Makulu wakiwemo wafugaji pamoja na wakulima wa maeneo hayo na viongozi wa Vijiji hivyo kukutana kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi.
Agizo hilo la diwani linatokana na kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara inayodaiwa kusababishwa na mwalimu wa shule ya msingi Chali Makulu aliyefahamika kwa jina moja la Mussa.

Hivi karibuni mwalimu Mussa alizua tafrani kwa kuwavamia wafugaji saba katika maeneo ya machungani na kushambulia watoto wa mitama na fimbo kwa madai kuwa wanalisha mifugo kwenye eneo lao licha ya kuwa uongozi unaeleza kuwa hautambuhi kama eneo hilo ni la mwalimu Mussa.
Kutokana na kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani Diwani amewaagiza viongozi wa eneo la Chikopelo, chali Makulu pamoja na viongozi wote wa wafugaji na wakulima kufika katika eneo la chambuli na Mkambala kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi inayoonekana kushamili.
Maagizo hayo ya Diwani yanatokana na kuwepo kwa baadhi ya wafugaji kumlalamikia mwalimu wa shule ya msingi chali Makulu Mussa kuwatoza faini ya shilingi milioni 2,100,000 kwa wafugaji 7 kwa madai ya kulisha majani katika maeneo yao jambo ambalo linazua mgogoro kati ya mwalimu Mussa na na wafugaji hao.

Hata hivyo Diwani wa Kata ya Chali amesema ili kutatua mgogoro huo ni kukutanisha pande zote mbili za wafugaji na wakulima.
Wafugaji hao ambao walitozwa faini ni Masanilo Balai ,Dasse Matana,Chilalaa Masemde,Zengo Senga ,Mboojee Kazungu,Kurwa Masingija.
Katika hatua nyingine wafugaji wa kijiji cha Chali Makulu wameeleza kuchoshwa na vitendo vya unyanyasaji ambavyo vinafanywa na Mwalimu huyo pamoja na kuwatishia maisha.
Kwa upande wake mwalimu Mussa ameeleza kuwa yeye analazimika kuwatoza faini wafugaji hao kwa kulisha mifugo yao katika maeneo yake.
Mwalimu Mussa aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa maeneo waliyolisha wafugaji hao ni eneo lake na kukuri kuwa aliwapiga watoto waliokuwa wakichunga kwa maelezo kuwa ilikuwa njia ya kuwapata wahusika waliowatuma kulisha mifugo katika eneo lake.
Mwenyekiti wa Kijiji cha chali Makulu Mtembezi Samamba anaeleza kuwa Mwalimu Mussa amekuwa akisogeza mipaka kwa ajili ya kujipatia eneo kubwa kinyume na utaratibu.
Naye mtendaji wa kijiji cha Chali Makulu Edson Benjamini ameeleza kuwa serikali imetoa mwongozo wa kusimamia matumizi bora ya ardhi hivyo mpango huo unatakiwa kutekelezwa kikamilifu.


More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina