May 14, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof.Mbarawa:Bandari ya Dar es Salaam imeimarika kwa ufanisi,ushushaji na upakiaji wa Kontena

Na Penina Malundo,Timesmajira

Waziri wa Uchukuzi,Prof.Makame Mbarawa,amesema kuwa tangu uwekezaji wa DP World kuwekeza katika bandari ya Dar es Salaam,imeweza kuchangia kuimarika kwa ushushaji na upakiaji wa kontena kwa wingi katika bandari hiyo.

Amesema kwa mwezi wa Disemba 2024 kontena takribani 18000 zimeweza kuhudumiwa katika bandari hiyo ,ukilinganisha na Mwaka 2025 mwezi huo ambapo takribani kontena 36000 zinaweza kuhudumiwa ambapo ni mara ya mbili ya mwaka 2024.

Akizungumza hayo jana jijini Dar es Salaam,wakati wa ziara yake akitembelea Bandari hiyo na Mradi wa ujenzi wa Bandari Kavu Kurasini,Prof.Mbarawa alisema wakati kitengo hicho cha makontena kikiwa chini ya Mamlaka ya Bandari (TPA ) kilikuwa utendaji wake upo chini .

Amesema changamoto kubwa iliyopo ni kutoa kontena katika eneo hilo na kupeleka eneo lingine la kuhifadhi makontena hayo ikiwemo ujenzi wa eneo laa mpango wa ujenzi wa bandari kavu wa EPZD.

”Hivyo Makontena haya yatakuwa yakishushwa hapana na kupelekwa katika eneo la EPZD alafu wadau na wateja watakuwa wanachukulia mizigo yao huko katika eneo hili hii inalengo la kuongeza ufanisi zaidi katika Bandari yetu kwani kumekuwa na ongezeko la kushusha Makontena mengi,”Anasema

Prof.Makame amesema uwepo wa uwekezaji wa DP World katika bandari ya Dar es Salaam imeleta faida kubwa kwa TPA kwa muda mrefu.”Awali kwa mwaka TPA ilikuwa inakusanya takribani Bilioni 700 hadi 800 ila kwa sasa hivi tumepokea tril 2.03 tangu wawekezaji waingie katika bandari hii,”alisema Prof. Makame

Alisema hatua hiyo ni kubwa na ni maendeleo makubwa kama nchi na hata kwa upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ushuru wa Forodha kupitia TRA umeweza kuongezeka kupitia uwekezaji huo.

Amesema tangu kuwepo kwa wawekezaji katika Terminal 1 na 11 zimeanza kufanya vizuri bandari ya Dar es Salaam imeweza kupiga hatua.

”Ni muhimu na kuendelea kuweka mazingira mazuri kufanyika kwa haya yote ni maendeleo makubwakuhakisha tunachangia uchumi wa nchi.

” Sisi tuliopewa dhamana ya kuendelea kuweka mazingira mazuri na kujenga miundombinu ya kutosha kuhakikisha bandari inafunguka na tunafaidia na uwekezaji huu na uchumi kwa ujumla,”amesema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam,Abed Gallus amesema katika Termina 1 kuna uwekezaji mkubwa umefanyika ambapo hadi sasa kuna mashine za kushushia makonterna zinazoitwa SSG tano na mashine ya RTG ambayo ni kazi yake ni kupokea mzigo inayotoka melini kuweka katika yadi na kutoka katika yad na kuwapa wateja.

”Mashine hizi zimeboresha utendaji kazi wabandari hii Dar hususan termina 1,utendaji umeboreka ndani ya siku tatu meli inakuwa imehudumiwa hii inamaanisha meli kuhudumiwa ikiwa gatini masaa 24 na tunauwezo wa kuhudumia hadi Kontena 1000 wakati mwanzo ilikuwa sio hivyo.

”Meli kusubiri nangani nayo imesaidia kupunguzwa muda kwani ikifika kwa sasa inaweza kuhudumiwa ndani ya wastani wa siku 5 ila mwanzoni ilikuwa zaidi ya siku 30,”alisema.

Naye Meneja Uhusiano wa DP World wa Ndani,Elitunu Mallamia amesema wao kama DP WORLD wameanza kutizama na kuona kwamba kuna ongezeko kubwa la mizigo inayokuja Bandari ya Dar es Salaam katika Termina 1.

”Tumefanya jitihada mbalimbali za kuweza kunasua hilo jambo na kuweza kuhimili huo mzigo ,tumewekeza kwenye geti jipya 4D kwaajili ya kuongeza uwezo wa mizigo kutoka bandarini na vifaa mbalimbali vya kuhudumia mzigo lakini tuliona kuna kasi ndogo ya uondoshaji wa mizigo kutokea kwenye maghala ya SD tukaona ili kuweza kusaidia wafanyabiashara wa kitanzania wasiweze kupata hasara kupita kiasi tuliona ni vizuri kutoa msamaha wa tozo wa uhifadhi kwa mzigo wowote ulioshuka kuanzia Januari mosi hadi Februari 5.

“Tumetoa siku tano kutokea Februari 6 hadi 10kwaajili ya SD kuondosha mzigo Bandarini pamojana na wateja “Wateja wanaoweza kutoa mzizigo yao bandarini tunawakaribisha na kuongeza kasi ya kuchukua kuweza kutumia kasi ya msamaha huu na kuongeza mzigo unaingia sokoni kwa lengo la kuchagiza biashara,”ameema.