March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Dkt.Samia ameagiza ulipaji kodi Kariakoo kwa kufuata mifumo

Na Heri Shaaban,Timesmajira

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,ameagiza ulipaji kodi katika soko la Kimataifa la Kariakoo ufuatwe kwa mifumo ya kazidata kwa ajili kukusanya mapato ya Serikali.

Dkt.Samia Suluhu Hassan, amesema hayo katika ufunguzi wa soko la Kariakoo Wilayani Ilala Mkoa Dar es Salaam ambapo soko hilo litatoa huduma kwa wafanyabiashara 1500.

“Naagiza ulipaji kodi katika soko hili la Kimataifa la Kariakoo utumike kwa kufuata mifumo ya kazidata uwazi wa mapato na matumizi uwepo ili kuiongezea mapato Serikali ” amesema Dkt.Samia.

Aidha ameagiza shirika la Masoko la Kariakoo kusimamia kupangisha wafanyabiashara wa soko hilo ambao wanaitaji maeneo ya Biashara sio Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.

Ameagiza Shirika la viwango Tanzania TBS na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania TMDA kusimamia ubora wa bidhaa katika soko hilo la Kariakoo uwe wa Kimataifa.

Kwa upande mwingine amemwagiza Mkurugenzi wa Shirika la Masoko Kariakoo kutenga eneo maalum la kulea watoto au sehemu ya kuwanyonyeshea watoto wa Wafanyabishara wa Kariakoo ndani ya soko hilo la Kimataifa.

Kwa upande mwingine Rais alizungumzia DAWASA maji safi na salama alisema maji kwa sasa yapo ya kutosha katika soko hilo la Kimataifa ambapo aliagiza kuwe na mfumo mzuri wa usafi ndani ya soko hilo na magari yote ya kushusha mizigo yawe yanaingia kwa utaratibu maalum.

Akizungumzia Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam amewagiza Ilala kukusanya mapato kwa ukamilifu na wale wasiolipa kodi wapewe muda waweze kulipa kwa wakati.

Mkuu wa mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila amesema jumla ya Wafanyabishara 1500 wanatarajia kufanya biashara katika soko hilo la Kariakoo,ambapo alitoa agizo kuanzia leo barabara zote za Kariakoo ziwe wazi marufuku kufunga barabara .

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila ameagiza Dipromasia itumike bila kutumia nguvu kubwa katika kuwaondoa wafanyabiashara barabarani Kariakoo.

Amesema jengo la DDC Kariakoo pia litatumika kwa ajili ya Wafanyabishara 500 kwa ajili kufanya biashara zao na kufuata taratibu.