Na Joyce Kasiki, Dodoma
MBUNGE wa Jimbo la Katoro, Mhandisi Kija Ntemi, ameihoji Serikali kuhusu upatikanaji wa huduma za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika jimbo la Katoro mkoani Geita.
Akiuliza swali Bungeni jijini Dodoma Mbinhe huyo Swali hilo lililenga kujua ni lini Serikali itapeleka gari la zimamoto Katoro ili kuwezesha utoaji wa huduma za haraka pindi dharura zinapotokea.
“Je ni lini Serikali itapeleka gari la zimamoto Katoro ili kuwezesha utoaji wa huduma za haraka pindi dharura zinapotokea.”
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ayoub Mohamed Mahmoud ameeleza kuwa, Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuliimarisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini.
Amesisitiza kuwa jitihada hizo ni sehemu ya mkakati mpana wa kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao unalindwa kwa ufanisi zaidi.
Naibu Waziri alifafanua kuwa Serikali imekuwa ikilipa kipaumbele suala la vitendea kazi kwa jeshi hilo, ikiwemo ununuzi wa magari ya kisasa ya kuzima moto na uokoaji hatua inayolenga kuongeza uwezo wa jeshi hilo kufika maeneo ya matukio kwa wakati na kutoa msaada unaohitajika haraka.
“Serikali ilitangaza kuwa Jimbo la Katoro tayari limepatiwa gari moja jipya la zimamoto na uokoaji aina ya IVECO. Gari hilo ni la kisasa na linatarajiwa kuboresha kwa kiasi kikubwa utoaji wa huduma za zimamoto katika eneo hilo.”alisema Naobu Waziri huyo
Kwa mujibu wa majibu wa Naibu Waziri Mahmoud, gari hilo kwa sasa lipo Mkoani Dar es Salaam likikamilishiwa taratibu za mwisho kabla ya kusafirishwa.
Naibu Waziri aliongeza kuwa gari la zimamoto linatarajiwa kufika Mkoani Geita 09 Februari, 2026 huku akisema kuwa, ujio wa gari hilo utaimarisha usalama wa wananchi wa Katoro na maeneo ya jirani, hasa katika kukabiliana na majanga ya moto na dharura nyingine.

More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama