March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Lukiza Autism yapongezwa kwa kubadili simulizi la changamoto ya usonji na kulipeleka kwenye utetezi 

Na Penina Malundo,Timesmajira 

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Women Fund Tanzania Trust na Mwanzilishi wa Taasisi ya Nendiwe Feminist&Wellness Centrel,Mary Rusimbi ameipongeza Taasisi ya Lukiza Autism kwa kazi kubwa iliyoifanya kwa Watanzania   kuonesha namna ya kubadili simulizi ya changamoto ya ukimya ya watoto wenye usonji na kupeleka katika suala la Utetezi na jumuishi wa pamoja.

Akizungumza hayo  jijini Dar es Salaam,wakati wa hafla ya Chakula cha Usiku ya Autism Awareness Charity Gala Dinner msimu wa nne na Kusherehekea miaka mitano ya kuanzishwa kwa Taasisi  hiyo ya Lukiza Autism,Rusimbi alisema taasisi hiyo ya Lukiza imetoa mchango mkubwa kwa jamii katika kubadili simulizi ya changamoto za watu hao.

Amesema awali watoto wenye usonji walikuwa wakifungiwa ndani ila baada ya elimu kubwa juu ya hali hiyo,watoto wameanza kuonekana katika vituo mbalimbali vya tiba na wengine kupelekwa katika Centa.

Amesema usonji sio suala la mtu binafsi anaepata changamoto ni suala la kijamii na kitaifa,hivyo jamii ikishirikiana kwa pamoja katika kutoa haki kwa watoto hao na kuhakikisha watoto hao wanatunzwa vizuri wanajenga taifa lenye nguvu kazi.

“Sasa ni wakati wa kuondoka na  dhana ya kusaidia watu wenye usonji kama huruma, badala yake ione ni suala la haki katika kutoa msaada  wao.

”Kuna pengo kubwa lililopo kati ya mahitaji halisi ya familia hizi zenye watoto wenye usonji na mifumo ya kijamii,na pengo hili lipo zaidi katika mahitaji halisi sio ya kifedha tu,”alisema

Rusimbi amesema kutokana na usonji kutoonekana ni hisani na kuwa haki hivyo wanapaswa kuhamisha ulezi wa mtoto kutoka kwa mama mmoja ,familia au taasisi na kuona jamii nzima wanawajibu zaidi.

”Tubadili hili na kuwa mfumo wa pamoja usimuachie muhusika pekee au serikali hili nijukumu letu waote kama taifa,”amesema 

Kwa Upande wake Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lukiza,Hilda Nkabe amesema hafla hiyo ya Chakula cha usiku ina malengo makuu matano ikiwemo kusherekea miaka mitano tangu kuanza kazi za taasisi ya Lukiza,kutoa tuzo kwa wadau mbalimbali ambao ambao wameleta mabadiliko chanya katika jamii kwa mwaka 2025,kuzindua rasmi mbio za Run 4 Autism 2026,Kuwapa nafasi wazazi na walezi muda wa kufurahi pamoja na wadau wengine wa usonji na maendeleo ya Jamii na Kuchangisha fedha kwaajili ya kuendeleza utekelezaji wa mradi wa miaka mitano wa Ustawi kwa kila mtoto viashiria vya Usonji.

Amesema miongoni mwa mafanikio ya taasisi ya Lukiza yaliyoyapata katika kipindi cha miaka mitano ni Kuelimisha jamii kuhusu hali ya usonji nchini Tanzania na kuhamasisha uwepo wa jamii jumuishi kupitia mbio ya Run 4 Autism Tanzania.

”Hadi sasa elimu ya uelewa wa usonji imewafikia takribani asilimia 30 ya Watanzania kupitia vyombo mbalimbali vya habari pia zaidi ya wanafunzi 250 wa chuo kikuu wanapata mafunzo ya fani ya mafunzo kuhudu huduma za utengamano,”amesema

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Lukiza,Dkt.Edward Kija amesema Taasisi ya Lukiza imekuwepo nchini kwa miaka mitano na imefanya kazi ya kuboresha ufahamu ili watoto wenye usonji wasiwekwe ndani watolewe na kupata huduma,kuhakikisha wanafikishwa katika vituo vya afya na ugunduzi kufanyika na kupata huduma wanazo stahiki.