March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Viongozi wa kisiasa na serikali waagizwa kutoa elimu ya Bima ya Afya kwa wote

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

WAZIRI Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba amewaagiza viongozi wote wa kisisasa na kiserikali kuendelea kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa bima ya Afya kwa wote ili waweze kujiunga na hivyo kuwa na uhakika wa matibabu.

Dkt.Nchemba alitoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilolo Dkt.Rita Kabati kwenye kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu.

Katika swali la Mbunge huyo alitaka kujua namna Serikali ilivyojipanga katika kutoa elimu ya Bima ya Afya kwa wote mpaka vijijini ili kila mtannzania anufaike na huduma za afya.

“Serikali imefanya kazi kubwa kupeleka huduma za afya mpaka vijijini lakini pamoja na upatikanaji wa huduma hizo kumekuwa na uelewa mdogo wa matumizi ya Bima ya Afya,je serikali imejipangaje kutoa elimu hiyo mpaka vijijini ili wananchi hao nao waweze kupata uelewa na kunufaika na mpango huo?”alihoji Dkt.Kabati

Akijibu Dkt.Nchemba alisema ,Bima ya Afya kwa wote ni hitaji la muda mrefu la wananchi ambalo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akaamua kupanua wigo katika uongozi wake kuanzia kipindi cha kwanza cha uongozi wake alielekeza kufuatwa kwa kwa taratibu zote za masuala ya sheria zikamilike.

“Ni kweli  hatua iliyosalia ni  ni ya kutoa elimu ,Bima ya Afya  ni msingi wa kuwezesha watanzania wote kuweza kumudu  gharama za matibabu kwa wale wenye uhitaji mkubwa wa matibabu na pengine hawawezi kabisa kuyalipia “alisema Dkt.Nchemba na kuongeza

“Jambo kubwa watanzania  tunalotakiwa kulifanya ni kujiunga katika vitita ambavyo vitaelekezwa na wizara na baada ya kujiunga Serikali inafanya kika jitihada kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa urahisi ,uhakika na kuokoa maisha yao.”

Aidha alisema  Rais Dkt.Samia aliahidi kuajiri wataalam wa afya  5,000 ndani ya siku 100 na tayari wameshaajiriwa na wamepelekwa katika zahanati,vito vya afya na hospitali zote nchini kwa lengo la kuhakikisha majengo yaliyojengwa kwa ajiki ya huduma za afya yapate wataalam wa afya wa kutosheleza.

Vile vile alisema hayo yote yanaenda sambamba na upatikanaji wa vifaa vya kisasa ambavyo vinapatikana katika hospitali zote nchini.

“Zamani vifaa kama CT Scan,MRI  vilikjwa vinapatikana Dar es Salaam pekee ,lakini sasa vinapatikana katika hospitali za Mikoa,hospitali za rufaa na Kanda.