Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
CHAPA za Yas na Mixx, zimesheherekea mwaka mmoja tangu zilipo jitambulisha upya sokoni mnamo Novemba mwaka 2024.
Sherehe hizo zinatambua ushirikiano na hatua zilizofikiwa katika safari ya mwaka mmoja kama mshirika wa kidigitali na huduma za kifedha kwa Watanzania.
Kwa mwaka mzima, Watanzania wamekuwa sehemu ya mabadiliko hayo yanayogusa si tu ukuaji wa mtandao na teknolojia, bali pia mahusiano ya watu, mafanikio ya pamoja na manufaa yanayoonekana katika maisha ya kila siku.

Hafla ya kusheherekea mwaka mmoja huo ilihudhuriwa na Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu – Zanzibar, Mudrick Soraga, ambaye alisisitiza umuhimu wa sekta binafsi katika kuisukuma Tanzania kwenye uchumi wa kidijitali.
Amesisitiza kuhusu ushirikiano na taasisi za sekta binafsi, Soraga aliishukuru Yas kwa kukubali kushirikiana na Wizara yake katika kuhakikisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Wananchi wake wananufaika na mageuzi ya TEHAMA.
“Zanzibar sasa hivi tupo katika safari ya kidigitali na ndio maana tumeona tutafute wadau ambao ni wabobezi katika mambo haya ya TEHAMA ili tuweze kushirikiana nao. Tunayo mipango mikubwa kuhakikisha Zanzibar inasonga mbele kidigitali,” amesema.
Akizungumzia kuhusu nafasi ya Yas na Mixx nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa AXIAN Telecom Group, Hassan Jaber, amesema:

“Mwaka mmoja uliopita tulizindua Yas na Mixx tukiwa na ndoto ya kuikuza kizazi cha kidijitali na kuunganisha jamii barani Afrika.
“Leo, tunapoadhimisha mwaka mmoja, ninafurahi kuona ndoto hiyo ikichukua sura halisi.Katika kipindi cha miezi 12, tumeboreshaji mtandao wetu, tumepanua huduma za 5G na Fiber, tumeongeza upatikanaji wa huduma za kidijitali na kuleta matokeo chanya kwa wateja wetu.
“Maono yetu bado ni yale yale, kuifanya Yas kuwa moja ya chapa imara zaidi barani Afrika, huku tukihakikisha maendeleo yanakuwa jumuishi na yanayochangia malengo ya muda mrefu na mabadiliko ya kidijitali nchini Tanzania,” amesema Jaber.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas- Tanzania, Pierre Canton Bacara, amewashukuru wateja, washirika, wafanyakazi na jamii kwa ujumla kwa kuufanya mwaka wa kwanza kuwa “mwaka wa mageuzi ya kweli

“Tunapoadhimisha mwaka mmoja wa Yas, tunawashukuru wote waliotembea nasi katika safari hii. Mwaka huu tumefanya uwekezaji wa zaidi ya TZS trilioni 1 katika kupanua na kuboresha mtandao wetu, na kuhakikisha tunawafikia wateja zaidi ya milioni 29.
“Lengo letu ni kuwa mshirika wa kweli wa kidijitali kuwawezesha vijana, wafanyabiashara, mashirika makubwa na hata taasisi za Serikali kufanikiwa katika dunia ambayo kila siku inazidi kukua kidijitali,” amesema.
Mbali na mtandao, Yas imekuwa mstari wa mbele katika miradi ya kijamii-ikiwemo kusaidia wanafunzi kupata vifaa vya kujifunzia kidijitali, kuwajengea uwezo wasichana katika masuala ya teknolojia, ujasiriamali, pamoja na miradi ya kuhifadhi mazingira vijijini na mijini.

Bacara aliongeza kuwa “Huu ni mwanzo tu.
Tunabaki na dhamira ya kupanua huduma, kuongeza ubora wa uzoefu wa kidijitali kwa kila Mtanzania, na kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya taifa letu”.
Kupitia kampeni yake ya Anzia Ulipo, Yas imeendelea kuwawezesha wafanyabiashara wadogo, kuwahamasisha vijana na kuongeza kasi ya ujumuishaji wa kidijitali nchini.
Inapoelekea kwenye mwaka wa pili wa ukuaji, Yas imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika kufikia uchumi wa kidigitali unaotegemea teknolojia.

More Stories
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi
Waziri Mkuu kuanza ziara mkoani Rukwa Marchi 8 Hadi 10
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani