Na Mwandishi Wetu,Timesmajira
DIWANI wa Kata ya Buyuni, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Jesca Msolla, ameahidi kushirikiana kwa karibu na uongozi wa Jiji hilo katika kuhakikisha wananchi wa Buyuni wanapata maendeleo wanayostahili katika kipindi chake cha miaka mitano ya uongozi.
Jesca ameyabainisha hayo Jijini Dar es salaam mara baada ya kuapishwa rasmi pamoja na madiwani wenzake, katika kikao cha kwanza Cha mabaraza la Madiwani kilichoenda sambamba na kumchagua Meya na naibu meya.
Jesca amesema atafanya kazi kwa karibu na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Nurdin Bilal Juma (Sheta), Naibu Meya Jonh Ryoba Mrema, pamoja na watendaji wa Halmashauri katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo.
“Ndugu zangu waandishi wa habari, leo tumemchagua Mstahiki Meya na Naibu wake, na sisi madiwani tumeapishwa rasmi. Hii ni hatua muhimu ya kuanza kushiriki kikamilifu katika Baraza la Madiwani kwa ajili ya kuwatumikia wananchi katika kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo,” amesema
Aidha , amewahakikishia wananchi wa Buyuni kuwa hawajakosea kufanya uamuzi wa kumchagua kuwa Diwani wao, akisema kuwa amejiandaa kikamilifu kushughulikia changamoto zinazowakabili ikiwemo miundombinu ya barabara, elimu, afya, maji na huduma nyingine za kijamii.

“Natamani kata ya Buyuni iwe na maendeleo makubwa, na hivyo mimi kama diwani nitahakikisha malengo hayo yanafanikiwa,” ameongeza.

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI