Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online-Nkasi
Afya ya akili ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha msongo wa mawazo kwa watumishi walio wengi hali inayochangia kushindwa kutekeleza majukumu yao vizuri.
Ili kuhakikisha tatizo hilo linadhibitiwa kwa Watumishi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa kwakushirikiana na Mtaalamu wa afya ya akili wilayani humo, wametoa mafunzo kwa watumishi wa Halmashauri hiyo ili kukabiliana na tatizo hilo.

Akizungumza katika mafunzo hayo,Mratibu wa Magonjwa yasiyoyakuambukiza wa Wilaya Nkasi,Richard Kauzeni, amesema kuwa lengo la mafunzo hayo kwa watumishi nikuwaelimisha ili waweze kujua changamoto chanzo,athari za msongo wa mawazo na namna ya kukabiliana nazo mahala pa kazi.
Amesema kwa sasa watumishi wengi wanakabiliwa na tatizo hilo mahala pa kazi, hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kutatua msongo wa mawazo.
Pia amesema, changamoto ya msongo wa mawazo kwa watumishi inasababisha kukosa morali hivyo kuwa na utendaji mbovu wa kazi na taasisi kupata hasara huku uzalishaji pamoja na utoaji huduma unakuwa sio rafiki au haukidhi matakwa ya wananchi na kusababisha Serikali kunyooshewa kidole.
Hata hivyo amesema yapo mambo kadhaa yanayo sababisha watumishi kupata msongo wa mawazo ikiwemo kuwa na mahitaji makubwa ya kupata vitu vingi kwa wakati mmoja kupita vipato vyao.
Kwa upande wake Kaimu Ofisa Utumishi,Emmanuel Shombe,kupitia mafunzo hayo amewataka watumishi kutotegemea mishahara pekee, badala yake wawe na vyanzo vingine vya mapato ili kuepukana na mikopo isiyo ya lazima ambayo husababisha msongo wa mawazo kwa watumishi.
Shombe amesema ili kuendelea kupeana elimu, zaidi kutakuwa na mwendelezo wa mafunzo ya aina hiyo pamoja na mafunzo ya matumizi sahihi ya fedha.

Nao baadhi ya watumishi walioshiriki mafunzo hayo akiwemo Renatus Danda na Abdul Mtani wamesema mafunzo hayo yamewajenga kwa asilimia kubwa kwani wamepata uelewa zaidi na watayafanyia kazi pamoja na kuwasaidia watu wengine.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako