Na Moses Ng’wat, Songwe.
Idara ya Uhamiaji mkoani Songwe inawashikilia raia saba wa Pakistan kwa tuhuma za kukiuka masharti ya viza walizopewa walipoingia nchini.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Novemba 22, 2025, Kaimu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Songwe, Mrakibu wa Uhamiaji, Rose Mulaga Magesa, amesema watuhumiwa hao ni miongoni mwa raia tisa wa Pakistan waliokamatwa Novemba 18, 2025 katika katika msako maalumu uliofanyika katika mji wa Tunduma, Wilayni Momba.
Magesa, amesema masharti ya visa yalielekeza raia hao kwenda jijini Dar es Salaam katika maeneo ya Mbweni kwa shughuli za matembezi, lakini waliondoka na kufika hadi mkoani Songwe kwa shughuli ambazo hazikuainishwa, huku raia wengine wawili wa nchi hiyo walikamatwa kwa kutokuwa na vibali vya kuingia nchini.
Magesa amewataja waliokiuka masharti ya viza pamoja na namba zao za pasipoti kuwa ni Khizar Hayat (JJ6171151), Muhammad Rehman Rasheed (GU9842383), Muhammad Raza (YB9899821),Araiz Chand (YB9899821), Ahmed Ali (TF1832401),Aqib Javed (GH8676622) na Mubashar Ali (YF796162).

Amesema watuhumiwa hao wanatarajiwa kusafirishwa kwenda Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi mara baada ya mahojiano ya awali kukamilika.
Katika hatua nyingine idara hiyo ilieleza kuwa katika operesheni maalumu iliyofanyika kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 21, 2025 katika maeneo mbalimbali ya mpakani Tunduma ilifanikiwa kunasa wahamiaji wengine haramu 31 wote wakiwa ni kutoka nchini Ethiopia

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi