Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekanusha taarifa inayosambaa mitandaoni ikidai kuwepo kwa maandamano, likiielezea kama uzushi unaolenga kuwapotosha wananchi na kusababisha vurugu pamoja na uvunjifu wa amani nchini.
Kupitia taarifa yake kwa umma,iliyosomwa na Kanal Bernard Mlunga imesema JWTZ limewataka watanzania kupuuza tangazo hilo na kuwa waangalifu dhidi ya upotoshaji unaofanywa kupitia mitandao ya kijamii.
Aidha, amesema jeshi hilo limekemea vikali tabia inayozidi kushamiri ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, hasa pale inapolihusisha Jeshi la Wananchi na masuala ya kisiasa kwa nia ya kupotosha na kuzua taharuki miongoni mwa wananchi.
Amesema JWTZ imeeleza kuwa litaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) katika kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaojihusisha na vitendo vya upotoshaji kupitia mitandao.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi