Na Penina Malundo,Timesmajira
KAMPUNI ya Entertainment Africa (Premier Bet) imesema kuwa inaendelea kusherekea mafanikio ya promosheni ya Reward Hub(Maskani Zawadi) iliyozinduliwa mwanzoni mwa mwaka huu kwa kurudisha furaha kwa wachezaji wao waaminifu na kuonyesha uwazi na msisimko unaopatikana kwenye michezo yao.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,Ofisa Masoko wa Premier Bet,Sechelela Jonathan wakati wa akiongea na waandishi wa habari juu ya uendelezwaji wa Promosheni yao ya Reward Hub alisema promosheni hiyo ilizinduliwa mwaka huu mwanzoni na inawawezesha wachezaji kupata point na sarafu kwa kila bashiri wanayoweka kupitia online ya tovuti yao katika kupandisha ngazi,kubadilisha challenge na kubadilisha sarafu hizo na kuwa zawadi kwenye duka lao la mtandao.
Amesema mbali na zawadi hizo pia zipo za kidigitali ambazo tayari zipo ofisini zikisubiri washindi wake.
Alitaja miongoni mwa zawadi hizo ambazo zitatolewa kwa washindi wenye bahati mara tu watakapokidhi vigezo vya Promosheni hiyo ni pamoja na Tayota Harrier ya mwaka 2016,Bajaji TVS King Deluxe 2025 ambazo zipo mbili,Pikipiki Boxer Mbili,Simu aina ya Apple iPhone 16 Pro Max,Pikipiki za Umeme mbili,Televisheni aina ya Hisense inch 55 Smart 4K ,Seti za Paneli za Jua mbili na Spika za Bluetooth speaker 5.

“Leo tunajivunia kuonesha zawadi hizi halisi ambazo ni sehemu ya zawadi ya Promosheni hiyo kwa kuzingatiasera ya uwajibikajiya Bodi ya Michezo ya KubahatishaTanzania,”amesema Sechelela.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni hiyo ya kubashiri ya Premier Bet,Joyce El Chwaifaty amesema promosheni hiyo imekuwa moja ya promosheni yao pendwa zaidi hadi sasa ikihamasisha ushiriki na kuwalipa wachezaji wanaoshiriki kwa viwango tofauti.

Amesema kupitia promosheni hiyo inatoa uzoefu wa uwazi na wa thamani kwa wachezaji wao ambao wanapata ponti na sarafu kwa kila bashiri.
“Wachezaji wanaweza kupata point 1 na sarafu 1 kwa kila dola 1 wanayocheza kwenye casino na point 5 na sarafu 5 kwa kila dola 1 wanayocheza kwenye michezo.

“Baada ya hapo,wanaweza kubadilisha sarafu zao walizokusanyww kwenye dukani lao mtandao na kuchukua zawadi wanazopendelea kama pesa taslim ,bashiri za bure,bonasi na zawadi halisi,”amesisitiza.

Naye Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania,Elibariki Sengasenga ameipongeza kampuni hiyo kwa kujitolea kwake katika uwazi ,ufuatiliaji wa kanuni na michezo yenye uwajibikaji.

More Stories
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi
Waziri Mkuu kuanza ziara mkoani Rukwa Marchi 8 Hadi 10