Na Patrick Mabula, TimesMajira Online, Kahama
WANAWAKE wameaswa kuacha tabia ya kuwanyonyesha akina baba kwa imani potofu kuwa maziwa yao yanatibu tatizo la nguvu za kiume kwani kufanya hivyo kunaathili ukuwaji wa mtoto na kuwanyima haki yako ya lishe kutoka kwa mama.
Wito huo umetolewa na mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto wa Halmashauri ya mji wa Kahama, Carolyne Marcel katika tamasha la kutoa elimu kwa akinamama wanaonyonyesha watoto wenye chini ya umri wa miezi kuhusu ya umuhimu wa kumnyonyesha mtoto anapozaliwa hadi miezi sita bila kumpatia chakula chochote.
Katika tamasha hilo lililoandaliwa na shirika la SHDEPHA+ katika mradi wake wa Tulonge Afya, Naweza amesema, tabia ya akinababa kunyonya maziwa ya akinamama imekuwa inazidi kuongezeka siku hadi siku na kuwataka kuacha kitendo cha kuwadekeza wanaume kufanya hivyo kunawakosesha haki ya mtoto na kunaathiri ukuaji wa wao.
“Akinamama mnaonyonyesha kiwango cha akinababa kunyonya maziwa ya mama kinaongezeka sana kwa hiyo nawaasa acheni tabia hiyo ya kuwanyonyesha kwa sababu kufanya hivyo kumekuwa kukuathiri ukuaji wa mtoto kutokana na kutonyonya ipasavyo maziwa ya mama,” amesema Marcel.
Kwa upande wao akinamama wa kata ya Mwendakulima , Halmashauri ya mji wa Kahama wanaopatia elimu kuhusu afya ya mama na mtoto na umuhimu wa kunyonyesha watoto anapojifungua hadi miezi sita ambao hawakutaka majina yao yatajwe walikiri kuwa tabia ya akinababa kunyonya maziwa yao imekuwepo na inazidi kuongezeka.
Kaimu Mratibu wa Elimu ya Afya kwa umma ngazi ya jamii (THPCO) kutoka Halmashauri hiyo,Vestina Mutakyahwa anayetoa elimu ya unyonyeshaji wa mtoto ipasavyo, amewataka akinamama kuzingatia elimu wanayopewa na wataalamu wa afya kuhusu umuhimu wa kuwanyonyesha watoto maziwa ya mama peke yake kwa miezi sita mfululizo bila kumpatia risha ya aina yoyote.
More Stories
RC Makongoro: Samia aungwe mkono nishati safi ya kupikia
TAKUKURU,rafiki yanufaisha wananchi Mwanza
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua