Na Bakari Lulela,Timesmajira
KITUO cha Sera za Kimataifa Afrika (CIP–Africa)kimefanya utafiti unao onesha kuwa asilimia 84.5 ya walioshiriki kura ya maoni wameonesha kumpigia kura mgombea urais wa chama cha Mapinduzi (CCM).
Vilevile utafiti huo umeonesha kuwa asilimia 3 watampigia kura mgombea urais wa Chama Cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA)na asilimia 3 kwa mgombea urais wa Chama Cha Wanachi(CUF),na asilimia 1.5 kwa mgombea wa Chama cha NCCR–Mageuzi,huku asilimia 8 wakisema kura yao ni siri.
Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo leo Oktoba 22,2025 jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa habari,Mkurungezi wa tafiti na uchapishaji CIP -Afrika,Thabit Mlangi asema kuwa kura hiyo ya maoni ilifanyika kati ya Septemba 30 hadi Oktoba 5, 2025 katika mikoa 19 ikiwemo 17 ya Tanzania bara na mikoa miwili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
“Utafiti huu ulilenga kupata taswira ya hisia za wananchi kuhusu uchaguzi mkuu wa Rais,wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 29, 2025″amesema Mlangi
Nakubainisha kuwa mikoa iliyoshiriki ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Kaskazini Pemba, Kaskazini Unguja,Kigoma,Kilimanjaro, Mara,Mbeya,Morogoro,Mtwara,Mwanza, Pwani,Ruvuma,Tabora na Tanga.
Mlangi amesema kwamba jumla ya wahojiwa wa utafiti huo ni 1,976 walioshiriki katika kura hiyo ya maoni, ambapo wanaume walikuwa 988 na wanawake 988,na kati yao,asilimia 29 walikuwa na umri kati ya miaka 18–25, asilimia 32 walikua na miaka 26–35, asilimia 13 wakiwa na miaka 36–45, asilimia 17 wakiwa na miaka 46–55 na asilimia 9 walikuwa na zaidi ya miaka 55.
Kwa upande wa elimu,amesema asilimia 14 walikuwa na elimu ya msingi, asilimia 57 elimu ya Sekondari,asilimia 28 elimu ya chuo na asilimia 1 walikuwa na elimu nyingine.
Aidha amesema kuwa utafiti huo ulitumia mfumo wa sampuli nasibu, unaotumika kisayansi duniani,unaosaidia kuongeza usahihi wa matokeo kwa gharama nafuu na kutoa fursa sawa kwa washiriki wote.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako