March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TTCL yaahidi kuendelea kutoa huduma Bora kwa Watanzania

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesema  litaendelea kutoa huduma zake  za kuaminika na zenye ubora wa hali ya juu na kuendelea kusikiliza maoni ya wateja sambamba na kuhakikisha kila mteja anapata thamani stahiki ya huduma anazostahili.

Akizungumza jijini Dar es salaam jana wakati wa kufunga wiki ya Huduma kwa wateja 2025, Kaimu mkurugenzi wa biashara  Humphrey Ngowi ameeleza kwa kuishukuru  michango ya wateja,wao wenye moyo wa ushirikiano na juhudi zisizochoka wakiwa na kauli mbiu ya “Mission Possible” ambapo watazidi kufanikisha makubwa katika siku zijazo.

“Wiki hii imetupa fursa adhimu ya kuthmini mafanikio yetu, kuainisha maeneo ya kuboresha na kujifunza njia Bora zaidi za kutimiza mahitaji ya wateja wetu.

Pia imekuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu na kuimarisha ari ya timu miongoni mwa wafanyakazi wetu, kuanzia walimu hadi wale wa ngazi za chini,” amesema Ngowi

Aidha Ngowi amesema kwa miaka msingi TTCL imeendelea kuwa nguzo ya mawasiliano nchini Tanzania, ikiendelea kutoa huduma muhimu zinazowaunganisha watanzania mijini na vijijini na katika dunia ya sasa inayobadilika kwa Kasi.

Amesema kueleza kwamba TTCL wanatambua haja ya kuboresha mifumo yao kwa kutumia teknolojia za kisasa na kuongeza thamani katika huduma wanazozitoa kila siku.

“Wiki hii ya huduma kwa wateja imeacha alama ya kudumu katika Shirika letu ambapo imekuwa fursa ya kukusanya mrejesho kutoka kwa wateja kwa kutambua mapungufu na kuandaa maboresho yanayolenga kukidhi mahitaji halisi ya wateja.

“Mwaka huu TTCL imeendelea kufanya maboresho makubwa katika mifumo yake ya mawasiliano kupitia miradi ya kimkakati ikiwa ni pamoja na kupanua Huduma mijini na vijijini, pamoja na kuendeleza upanuzi wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano na kusimamia ujenzi wa minara mipya,”amesisitiza

Maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa wateja yalianza rasmi Oktoba 6 mwaka huu na yamehitishwa jana Oktoba 10, 2025 na kudhibitisha na kaulimbiu ya “mission possible” si kauli mbiu tu bali ni uhalisia tunaouishi kila siku.