Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa amesema Uendeleeaji wa Bonde la Mto Msimbazi uanze sasa na uende sambamba na ulipaji wa fidia kwa Wananchi wote waliokubali kulipwa na kufanyiwa uhakiki wa Taarifa zao za Kibenki ili kupisha utekelezaji wa mradi huo.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo wakati alipofika kuzungumza na Wananchi wanaoathiriwa na Uendelezaji wa Bonde la Mto Mzimbazi leo tarehe 15.11.2023 kwenye eneo la Jangwani Jijini Dar es salaaam.
Amesema “leo hii nimekuja hapa kutoa Tamko ya hatua ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi uanze mara moja kuanzia sasa na hii iende sambamba na ulipaji wa fidia kutokana na tathmini iliyofanywa na wataalam.”
“Na mimi natambua kabisa wapo wananchi asilimia 92 kati ya wote wanatakiwa kulipwa fidia wanasubiria fedha zao na sikatai wapo wengine wenye malalamiko moja mbili tatu sikatai Wataalam wangu endeleeni kuyafanyia kazi na mkishindwa yaje kwangu nione hatua ya kuchukua.”
“Wale waliopo tayari hao walipwe fedha zao mara moja fedha zipo na tayari ameshatupatia Mhe. Rais kwa ajili ya ulipaji wa fidia za namna mbalimbali.”
“Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema hapa Katika Misingi ya ukaaji kwenye maeneo wa hatarishi Sheria inaondoa ulipaji wa fidia kwa wakazji wa maeneo hayo lakini Mkuu wa Mkoa na Mhe. Diwani wamewaombea na kusema hili haliwezekani wananchi wetu tunaomba walipwe hata kifuta Jasho namimi nikazungumza na Mhe. Rais na akaridhia kila mmoja alipwe kifuta Jasho cha Shilingi Milioni 4.”
Akizungumza Katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaa Mhe. Albert Chalamila amesema kwa wale wote watakao kuwa na jambo watakuja kuniona mimi nitawasikiliza na lile litakalohitaji kupelekwa kwa Mhe. Waziri nitawapeleka alisisitiza.
Naye Mratibu anayesimamia Miradi inayotekelezwa na Benki ya Dunia Eng. Hamphrey Kanyeye amesema Wananchi wa Mitaa 16 watalipwa malipo mbalimbali kutokana na thamani ya vitu walivyonavyo.
Malipo hayo yatakumuisha Kifuta Jasho, Usumbufu, Mali pamoja na kodi ya nyumba ya miaka mitatu kwa wale wananchi waliokua na nyumba eneo hilo na wanaishi ili wapate fedha za kulipia kodi ya nyumba kipindi wanaendelea na ujenzi.
Ofisi ya Rais TAMISEMI inatekeleza mradi wa uendelezaji wa Bonde la Msimbazi kwa lengo la kukabiliana na mafuriko na kuboresha matumizi ya ardhi katika eneo la chini la bonde.
Mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia (WB), ambayo imeidhinisha Dola za Marekani 260 milioni (karibu Sh598 bilioni), huku Sh600 bilioni nyingine zikitolewa na Hispania na Uholanzi.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa