Na Joyce Kasiki, Timesmajira Online Geita
MKURUGENZI wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Hamid Mbegu limewataka wachimbaji wa Madini wakubwa na wadogo pamoja na makampuni yanayojihusisha na ugomboaji na uondoshaji wa shehena, kutambua kuwa jukumu la kuondoa shehena hizo, hususan zenye kemikali hatarishi, ni la TASAC pekee.
Mkurugenzi hugo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye maonyesho yabteknolojia ya Madini yaliyofanyika mkoani Geita kwa muda wa siku 10 tangu Septemba 18 hadi Septemba 28, 2025 katika viwanja vya Suluhu Hassan vilivyopo eneo la Bombambili.
Mbegu amesema kuwa baadhi ya makampuni yamekuwa yakisafirisha kemikali hatarishi kama Sodium Cyanide kupitia kampuni binafsi kwa ajili ya matumizi ya ulipuaji migodini, hali ambayo ni kinyume na sheria na taratibu za nchi.
Ameeleza kuwa ni lazima kemikali na vilipuzi vinavyotumika kwenye migodi visafirishwe na kuondolewa na wataalamu wa TASAC pekee kwa mujibu wa sheria, akisisitiza kuwa usimamizi huo ni kwa lengo la kulinda usalama wa watu na mazingira.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 7 cha Sheria ya Uwakala wa Meli, Sura ya 415, TASAC ndiyo taasisi pekee ya serikali iliyopewa mamlaka ya kusimamia shughuli zote za ugomboaji na uondoshaji wa shehena hatarishi kama baruti na kemikali zinazotumika katika uchimbaji na usafishaji wa madini nchini.
“Baadhi ya shehena hizi ni sumu na zina madhara makubwa. Hivyo Serikali kupitia TASAC inapaswa kusimamia kwa ukamilifu uondoaji wake ili kuzuia athari kwa binadamu na mazingira,” amesema Mbegu.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi