March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DCEA yanasa watuhumiwa 940 na dawa za kulevya

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), imewakamata watuhumiwa 940 wakihusishwa na tuhuma za kusafirisha na kusambaza dawa za kulevya nchini.Watuhumiwa hao wanahusishwa katika matukio yaliyofanikisha ukamataji wa kilogramu 33,077.623 za dawa za kulevya aina mbalimbali.

Hayo ameyasema jana, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ‘DCEA’, Aretas Lyimo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema, kati ya dawa hizo ambazo zilikamatwa katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba, 2025, ni kilogramu 4,553 zilikuwa mbegu za bangi.

Kamishna Lyimo amesema kupitia operesheni maalum iliyoendeshwa na mamlaka hiyo, pia waliteketeza ekari 64 za bangi.Pia, amesema wamekamata silaha mbili za moto aina ya gobore na bastola ikiwa na risasi 11, magari tisa, bajaji mbili na pikipiki 26 zilizohusishwa kwenye uhalifu huo.

Aidha, amesema katika operesheni iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika Mtaa wa Tupendane uliopo Manzese wilayani Ubungo walikamata watu watatu akiwemo raia wa Lebanon.

Amesema, watuhurniwa hao walikuwa na kilogramu 2.443 za dawa z kulevya aina ya Cocaine.”Dawa hizi ziliingizwa nchini kutokea nchini Brazil kupitia nchini Kenya hadi Uganda na baadaye Tanzania kwa njia za vipenyo,” amesema.

Kamishna Jenerali Lyimo amesema, katika tukio lingine jijini Dar es salaam, kwenye klabu ya “Bad London” iliyopo Temeke kwa Azizi Ally na klabu ya “Sanaa” katika eneo la “Reggae bar” iliyopo Masaki, walikamata sigara za kielektroniki (e cigarette) pisi 50 zilizotengenezwa kwa bangi zenye ujazo wa mililita 10 kila moja.Sigara hizo za kielekroniki zilizotengenezwa kwa kutumia kemikali pamoja na skanka ziliingizwa nchini kutokea Uingereza.

Miongoni mwa Kemikali hatarishi kwenye bangi hizo ni pamoja na THC, benzene na madini ya cadmium, lead, na mekyuri.”Kemikali hizo pamoja na madhara mengine ya kiafya, huweza kusababisha magonjwa ya akili, saratani, kuharibu mimba kwa mama wajawazito, kuathiri maendeleo ya ukuaji wa mtoto akiwa tumboni,”Lakini pia husababisha udumavu wa akili baada ya mtoto kuzaliwa na hivyo kuathiri uwezo wa kujifunza pamoja na uraibu,” amesema.

Aidha, katika eneo la Bahari Beach, Kamishna Lyimo amesema, walimkamata raia wa Marekani na mke wake raia wa Tanzania wakiwa na chupa 11 za dawa ya kulevya aina ya Ketamine pamoja na bangi na hatua za kisheria zinaendelea dhidi yao.Vilevile, kupitia kampuni za usafirishaji vifurushi jijini Dar es salaam, wamewakamata watu wanne kwa kukutwa na kilogramu 10.37 za mirungi wakiwa kwenye hatua za kuisafirisha kwenda nje ya nchi huku ikiwa imefichwa kwenye vifungashio vyenye chapa ya bidhaa za chai,kwa lengo la kukwepa kubainika.

Kadhalika, kupitia mifumo ya ufuatiliaji ya kimataifa katika kuzuia uchepushwaji wa kemikali bashirifu kutumika kutengeneza dawa za kulevya, Kamishna Jenerali Lyimo amesema, walizuia uingizwaji nchini lita 69.8 za kemikali aina ya Methyl ethyl ketone (MEK) na Ephedrine ambazo zilikuwa ziingizwe hapa nchini kinyume na taratibu.

Kupitia operesheni zilizofanyika mkoani Mara, walimkamata mhalifu kinara wa uzalishaji na usafirishaji wa bangi aitwaye Masero Ryoba Muhabe (44) akiwa na tani 6.5 za bangi.Amesema, kwa muda mrefu, Muhabe alikuwa akijihusisha na uzalishaji na biashara ya bangi wilayani Tarime Mkoani Mara na kusafirisha ndani na nje ya nchi.

Katika tukio lingine mkoani humo, Kamishna Lyimo amesema walimkamata Simoni Gervas Mkonda (51) akiwa na kilogramu 193 za bangi pamoja na silaha aina ya bastola ikiwa na risasi 11 ambayo amekuwa akiimiliki kinyume cha sheria akiitumia kulinda biashara zake haramu.

Aidha, mkoani Mbeya,waliwakamata Henry Shao (36) na Veronika Samumba (31) wakiwa na biskuti 241 zilizotengenezwa kwa bangi..”Watajwa ni wahandisi na wafanyakazi wa kampuni binafsi za ujenzi za HSS Engineering Company Limited na JIC Company Limited za jijini Mbeya.

“Baada ya upekuzi eneo la mtaa wa Forest watuhumiwa walikutwa na vifaa wanavyovitumia kutengeza biskuti hizo па kueleza kwamba waleja wao wakubwa ni wahandisi na vijana wa vyuo na mitaani.

“Pia, mkoani Mwanza, walikamata zaidi ya watuhumiwa sita wakiwa na kilogramu 452 dawa za kulevya aina ya bangi zikisafirishwa na gari aina ya Scania namba T 384 BWN likiwa na tela nambaT.602 ANQ mali ya Kampuni ya Coca Cola ya Nyanza iliyopo Mwanza, pamoja na bajaji mbili zilizokuwa zinabeba bangi hizo kutoka kwenye gari tajwa.

Vilevile, kupitia operesheni walizozifanya katika Mikoa ya Mara, Tabora, Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Ruvuma na Mo walikamata kilogramu 25,919.8 za mirungi, skanka na Heroine, kilogramu 4, mbegu za bangi na kuteketeza ekari mashamba ya bangi.

“Tunaendelea kuvunja mitandao ya dawa za kulevya na kubaini mbinu mpya za biashara na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo kuongeza wigo wa utoaji elimu juu ya matumizi ya dawa za kulevya, lengo likiwa ni dhamira ya Taifa katika kulinda usalama, kujali utu, watanzania, hatimaye kujenga stawi wa Taifa letu,” amesema Kamishna Jenerali