Na Bakari Lulela ,Timesmajira
Mtia nia wa Ubunge Jimbo la Temeke kupitia chama cha Mapindizi (CCM)Jasdeep Sindgh ameahidi kuleta Mabadiliko makubwa mara tu atakapopata ridhaa ya kuchaguliwa nafasi hiyo kwa kuwatumikia watanzania.
“Nimejenga vyumba nane katika wodi ya wazazi kwa ajiri ya wakina mama kwenda kujifungulia kwa pesa binafsi, nimejenga jiko katika shule za misingi ambalo linahudumia watoto 1500 bila michango ya wazazi wao , nimejenga maktaba kwa shule ya sekondari kwa ajiri ya wanafunzi wetu kwa ajiri ya kujisomea”Amesema JASDEEP
Aidha mtia nia huyo SINGH eliendelea kwa kusema ametoa kadi za bima ya afya kubwa kutoka ufadhili wa ubalozi wa Marekani takribani kaya 77sawa na watu 560 .
Sanjari na hilo alipongeza ilani ya chama cha mapinduzi ( CCM) kwa kuleta dira ya maendeleo ya mwaka 2050 hivyo itapelekea kuleta viongozi waadilifu, wachapa kazi wawazi na kuleta uongozi ambao unaleta maendeleo katika jamii zetu.

More Stories
Silinde azindua baraza la sita la Wafanyakazi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
NMB ilivyosaidia Serikali kukusanya zaidi ya Sh trilioni 9.8
Serikali yaongeza nguvu kwa wachimbaji wadogo,yasisitiza usalama Migodini