Na Yusuph Mussa,Timesmajiraonline,Kilindi
WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Kilindi katika kipindi cha mwaka 2025/2026 inatarajia kutumia jumla ya sh. 5,298,520,000 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ukarabati wa barabara, maendeleo na uendeshaji wa ofisi.
Hayo yamesemwa Januari 29, 2025 na Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilindi Mhandisi Martin Mwashambwa kwenye kikao cha Baraza la Bajeti la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi.
“Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2025/2026, Wakala inatarajia kutumia jumla ya sh. 5,298,520,000 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ukarabati wa barabara, maendeleo na uendeshaji wa ofisi.
“Kati ya fedha hizo, sh. 879,470,000 ni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya barabara kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara “Ukarabati” (Road Fund Maintenance), na sh. milioni 950 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya barabara kwa kutumia fedha za maendeleo “Fedha za Majimbo” (Consolidated Fund)” amesema Mhandisi Mwashambwa.
Mhandisi Mwashambwa amesema sh. 1,312,825,000 ni kwa ajili ya utekelezaji miradi ya maendeleo kupitia fedha za Mfuko wa Barabara “Maombi Maalumu” (Road Fund Development), na sh. 206,225,000 ni kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa ofisi.
Katika baraza hilo, bajeti tatu zimesomwa ikiwemo bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi, bajeti ya Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kilindi, na hiyo ya TARURA.
More Stories
Premium Active Tanzania yapunguza uhaba wa madawati Mlele
Madiwani Kilindi wapitisha bil.36.8 bajeti 2025/26
THBUB yatoa tamko kulaani mauaji ya Jumanne Juma