Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Januari 08 2025, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Kamati ya Kupambana na Udhalilishaji Zanzibar.
Ujumbe huo ulioongozwa na Mwenyekiti wake, ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, Bi. Mwanamkaa Abdulrahman Mohammed, umefika Ofisini kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, kwaajili ya kuwasilisha Taarifa ya Mwenendo wa Udhalilishaji Nchini, pamoja na kupata ushauri kutoka kwa Mheshimiwa Othman.
Ujumbe aliofuatana nao Bi. Mwanamkaa, umewajumuisha pia Maafisa kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, wakiwemo Bw. Mohamed Kassim Hassan na Ostadh Abdulkarim Said Abdulla.
More Stories
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango
LALJI yatoa msaada wa sare na vifaa vya shule kwa yatima