Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
MAMA mzazi wa aliyekuwa nyota wa filamu Tanzania Steven Kanumba , Florah Mtegoa, amesema hatua ya wasanii kuandaa tukio la kuwaenzi wasanii waliofariki limempa faraja kubwa hasa wakati huu wa miaka 12 ya kifo cha mwanaye Kanumba.
Flora ambaye pia amepoteza mtoto wake wa kiume Seth ambaye ni mdogo wake Kanumba, amesema ni kwa miaka mingi wasanii hawajawa na tukio kama hilo.
“Ninampongeza sana Steve Nyerere kwa kuandaa jambo hili la kuwaenzi wenzetu waliotangulia mbele za haki.Limenipa faraja kubwa ,”amesema.
Wasanii nchini leo wanafanya tamasha maalumu la kuwakumbuka wasanii, wanamichezo na watangazaji nyota waliofariki, katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

More Stories
TTB yaeleza Utalii wa michezo unavyochangia uchumi wa jamii
Rais Samia apongeza tuzo wafanyakazi bora ,JOWUTA yawatunza waandishi sita
Watumishi MZRH wang’ara maadhimisho Mei Mosi