Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wakati akimsikiliza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye kuhusu Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini wa 2Afrika kabla ya kuuzindua katika Kituo hicho cha Kampuni ya Mawasiliano na Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania kilichopo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye wakati akielekea kuzindua Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika cha Kampuni Mawasiliano na Simu za mkononi ya Artel Tanzania kilichopo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria uzinduzi wa Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Airtel Tanzania katika hafla iliyofanyika Kituo cha Mkongo wa Mawasiliano Baharini cha Kampuni ya Airtel Tanzania kilichopo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika kilichopo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023. Wengine pichani ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Airtel Afrika Dkt. Olusegun Ogunsanya, Mtendaji Mkuu wa Airtel Tanzania Dinesh Balsingh pamoja na viongozi wengine wakishuhudia. Viongozi mbalimbali wa Serikali na Sekta Binafsi wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika pamoja na Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wakimuangalia Msanii Mrisho Mpoto alipokuwa akitumbuiza kwenye kwenye hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika pamoja na Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwa njia ya Mtandao na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika pamoja na Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Mawasiliano ya Artel Tanzania iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa nembo ya 5G kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Airtel Afrika Dkt. Olusegun Ogunsanya mara baada ya uzinduzi uliofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023. Roboti akiwa amebeba nembo ya 5G mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Airtel Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023. Post Views: 532 Continue Reading Previous UWAMARAUDAR waiomba Serikali iwatambueNext Zambia kushirikiana na hospitali ya rufaa ya kanda ya Mbeya utoaji huduma za afya More Stories Habari FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu December 25, 2024 Penina Malundo Habari Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake December 25, 2024 Judith Ferdnand Habari Kitaifa Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba December 24, 2024 Abdallah Mashaka
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba