November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa tasnia ya pamba Tanzania yenye kauli mbiu"zalisha pamba kwa tija na ubora kuongeza kipato na kufikia uchumi wa viwanda" uliofanyika Mkoani Mwanza. Picha na Judith Ferdinand, TimesMajira

Waziri Hasunga ataka wakulima kulima kilimo cha kisasa

Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema wakulima wanatakiwa kuhamasishwa kujikita na kufuata maelekezo ya kilimo cha kisasa.

Wito huo umetolewa leo jijini Mwanza na Waziri Hasunga wakati wa mkutano maalumu wa wadau wa tasnia ya pamba wenye Kauli Mbiu isemayo zalisha pamba kwa tija na ubora kuongeza kipato na kufikia uchumi wa viwanda.

Hasunga amesema, wakulima wanapaswa kuhamasishwa kwenye kilimo cha kisasa ili kuongeza uzalishaji kwa kutumia pembejeo bora ikiwemo mbegu na viuatilifu zinazoongeza uzalishaji pamoja na teknolojia ya kisasa ambayo mkulima ataweza kupata kilo 1,350 kwa hekari moja kama nchi nyingine zinazolima pamba .

Anesema ifike mahali zao la pamba liwe linachakatwa ndani ya nchi kwa kuhakikisha viwanda vinafufuliwa na watu wanawekeza ili kuwe na uhakika wa soko.

“Asilimia 65 ya viwanda vinategemea malighafi kutoka kwenye kilimo, hivyo lazima tuwezeshe mfumo wa kilimo wa kisasa, kwani kilimo ndio kinatupatia asilimia 100 ya chakula,” amesema Waziri Hasunga.