Na Esther Macha, Timesmajira,Online,Mbeya
ALIYEKUWA Mbunge mstaafu wa jimbo la Mbarali na Mwekezaji wa kampuni ya Mbarali Estate,Haroon Mulla Pirmohamed amechukua fomu ya kugombea nafasi ujumbe wa halmashauri kuu ya taifa (NEC)kupitia mkoa wa Mbeya .
Fomu hiyo amekabidhiwa leo na Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM)mkoa wa mbeya ,Mwalimu Shaibu Akwilombe.
Aidha Akwilombe amesema kwa nafasi za juu za chama kwa upande wa nafasi ya Mwenyekiti wa mkoa waliochukua ni watu watatu akiwepo Mwenyeiti wa aliyemaiza muda wake Mchungaji Jacob Mwakasole.
Kwa upande wa nafasi ya halmashauri kuu Taifa (NEC) Mkoa wa Mbeya idadi ya walichukua fomu ni watu wanne akiwepo Mwekezaji huyo na Mkurugenzi wa Shule za Paradise na Patrick Mission Ndele Mwaselela,
Alibainisha kuwa kwa nafasi ya Katibu wa siasa na uenezi mpaka sasa ni watu watatu akiwepo anayetetea nafasi yake Bashiri Madodi .
Hata hivyo Katibu huyo amesema kuwa wanachama wanaendelea kuchukua fomu kuwania nafasi mbali mbali za uongozi ndani ya chama.
More Stories
Mwanasheria Mkuu apiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa
CHADEMA yasikitishwa mawakala wao kuzuiliwa
Rais Samia amlilia Dkt. Ndugulile