Na Penina Malundo,timesmajira,online
SERIKALI imetakiwa kuwajengea uwezo na mbinu za ziada walimu nchini katika kuwatambua na kuwafundisha watoto wenye Usonji.
Aidha Walimu wakijengewa uwezo na kupatiwa mbinu hizo za ziada kwa kiasi kikubwa wataweza kuwasaidia Watoto wenye usonji kukaa darasani kwa utulivu,kuelewa na kutoona kero.
Akizungumza hayo leo jijini Dar es salaam,Daktari Bingwa wa Afya na Magonjwa ya Akili wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),Dkt. Saidi Kuganda amesema walimu wakiwezeshwa na kujua namna ya kufundisha Watoto wa namna hiyo inasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la Watoto hao.
Amesema ufundishaji wa walimu ni moja ya mbinu ya tiba nzuri ambayo itasaidia kupunguza tatizo la Watoto hao nchini.
“Hatuna data kamili ila tatizo lipo na tunaliona ukiliwahi mapema unapunguza kwa kiasi kikubwa madhara yake,ila ukiyaacha na kuchelewa yatakuwa makubwa pindi mtoto anapokuwa,”Amesema
Aidha amesema walimu hao wakiwekewa utaratibu mzuri katika kuwafundisha Watoto hao ni rahisi kuwasaidia katika ukuaji wao.
“Nchi nyingi zinafanya hivyo katika kuhakikisha walimu wanajengewa uwezo na mbinu za ziada za kuwafundisha watoto ikiwemo nchi ya Japan wao wanashughulikia walimu na sio madaktari kwani walimu wanambinu nyingi za ziada,”alisema
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lukiza Autism,Hilda Nkabe amesema usonji hauna dawa ila kuna mazoezi tiba ambayo yanasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza makali ya ugonjwa.
Amesema mzazi,mlezi na Familia ya mwenye mtoto mwenye usonji wanapaswa kuwa na upendo unaweza kusaidia kupunguza ukali wa ugonjwa huo kwa mtoto.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Dr.Reginald Mengi ,Shimimana Ntuyabaliwe amesema ni vema jamii kumtambuliza jamii kwa utu wake na sio kwa ulemavu aliokuwa nao.
Amesema utumiaji wa lugha sahihi kwa watu hao itaondioa Imani potofu na kuheshimu utu wa watu wenye ulemavu .
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito