Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mkurugenzi Mkuu wa Fedha wa Yas Tanzania, Innocent Rwetabura, amesema kampuni hiyo imewekeza zaidi ya shilingi trilioni 1.2 katika kipindi cha miaka minne iliyopita ili kupanua upatikanaji wa teknolojia za kisasa za mawasiliano, ikiwemo mtandao wa 4G na 5G, hatua inayochochea mageuzi katika utoaji wa huduma za afya nchini.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Hayati Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, Rwetabura alisema matumizi ya teknolojia ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hususan katika kuboresha mifumo ya taarifa za afya, huduma za afya kidijitali na kufanya maamuzi yanayotegemea takwimu sahihi.
“Tayari tumeona matokeo chanya ya matumizi ya teknolojia katika afya. Kuna tiba kwa njia ya mtandao (telemedicine), uchunguzi wa magonjwa kwa njia za kidijitali, mafunzo endelevu kwa wataalamu wa afya pamoja na huduma za dharura zinazowafikia wananchi kwa haraka zaidi,” alisema Rwetabura.

Alisema mafanikio hayo yamechangiwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni za mawasiliano, huku Yas Tanzania ikiwa imewekeza zaidi ya shilingi trilioni 1.2 katika kipindi cha miaka minne iliyopita ili kuhakikisha huduma za mtandao wa 4G na 5G zinawafikia Watanzania katika maeneo mbalimbali ya nchi.
“Kadiri teknolojia inavyoendelea kubadilisha utoaji wa huduma za afya, ndivyo inavyofungua fursa kwa watu wengi zaidi kushiriki katika safari hii ya mabadiliko. Leo tunashuhudia vijana wabunifu, wahandisi na wajasiriamali wa kijamii wakitumia teknolojia kutatua changamoto halisi zinazokabili sekta ya afya,” alisema.

Rwetabura alisema kauli ya Hayati Rais Benjamin Mkapa kwamba “mustakabali wa nchi uko mikononi mwa vijana” inaendelea kuthibitishwa na mchango wa vijana wanaotumia teknolojia za kidijitali kuibua suluhisho bunifu katika sekta ya afya.
“Hatuwezi kuzungumzia urithi wa Rais Mkapa bila kutambua imani yake katika ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kama nyenzo muhimu ya kuharakisha utoaji wa huduma bora za afya,” alisema.

Alisema Yas imeendelea kuunga mkono juhudi hizo kupitia ushirikiano na Serikali na wadau mbalimbali, ikiwemo RITA na UNICEF katika usajili wa vizazi kwa watoto walio chini ya miaka mitano, ambapo zaidi ya watoto milioni 13 walipata usajili na vyeti vya kuzaliwa kupitia mfumo wa SMS.
“Pia tumeshirikiana na Hospitali ya CCBRT kusaidia matibabu ya watoto wenye tatizo la miguu ya kupinda (clubfoot), na tunaendelea kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya macho bure Tanzania Bara na Zanzibar ambapo tayari tumewafikia Watanzania zaidi ya 23,000,” alisema.
Rwetabura alisema Yas ipo katika mazungumzo na Taasisi ya Benjamin William Mkapa kwa lengo la kuanzisha ushirikiano wa kimkakati utakaosaidia kuendeleza miradi endelevu ya afya na maendeleo kwa wanawake, watoto na vijana.
“Yas itaendelea kuwa mshirika katika safari hii kwa kuwekeza katika suluhisho bunifu za teknolojia zitakazoimarisha mifumo yetu ya afya na kuwawezesha vijana kuleta mageuzi katika utoaji wa huduma za afya. Kwa pamoja tunaweza kujenga Tanzania yenye afya bora zaidi, iliyounganishwa zaidi na yenye ustahimilivu zaidi,” alisema Rwetabura.
Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mkurugenzi Mkuu wa Fedha wa Yas Tanzania, Innocent Rwetabura, amesema kampuni hiyo imewekeza zaidi ya shilingi trilioni 1.2 katika kipindi cha miaka minne iliyopita ili kupanua upatikanaji wa teknolojia za kisasa za mawasiliano, ikiwemo mtandao wa 4G na 5G, hatua inayochochea mageuzi katika utoaji wa huduma za afya nchini.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Hayati Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, Rwetabura alisema matumizi ya teknolojia ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hususan katika kuboresha mifumo ya taarifa za afya, huduma za afya kidijitali na kufanya maamuzi yanayotegemea takwimu sahihi.
“Tayari tumeona matokeo chanya ya matumizi ya teknolojia katika afya. Kuna tiba kwa njia ya mtandao (telemedicine), uchunguzi wa magonjwa kwa njia za kidijitali, mafunzo endelevu kwa wataalamu wa afya pamoja na huduma za dharura zinazowafikia wananchi kwa haraka zaidi,” alisema Rwetabura.
Alisema mafanikio hayo yamechangiwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni za mawasiliano, huku Yas Tanzania ikiwa imewekeza zaidi ya shilingi trilioni 1.2 katika kipindi cha miaka minne iliyopita ili kuhakikisha huduma za mtandao wa 4G na 5G zinawafikia Watanzania katika maeneo mbalimbali ya nchi.
“Kadiri teknolojia inavyoendelea kubadilisha utoaji wa huduma za afya, ndivyo inavyofungua fursa kwa watu wengi zaidi kushiriki katika safari hii ya mabadiliko. Leo tunashuhudia vijana wabunifu, wahandisi na wajasiriamali wa kijamii wakitumia teknolojia kutatua changamoto halisi zinazokabili sekta ya afya,” alisema.
Rwetabura alisema kauli ya Hayati Rais Benjamin Mkapa kwamba “mustakabali wa nchi uko mikononi mwa vijana” inaendelea kuthibitishwa na mchango wa vijana wanaotumia teknolojia za kidijitali kuibua suluhisho bunifu katika sekta ya afya.
“Hatuwezi kuzungumzia urithi wa Rais Mkapa bila kutambua imani yake katika ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kama nyenzo muhimu ya kuharakisha utoaji wa huduma bora za afya,” alisema.
Alisema Yas imeendelea kuunga mkono juhudi hizo kupitia ushirikiano na Serikali na wadau mbalimbali, ikiwemo RITA na UNICEF katika usajili wa vizazi kwa watoto walio chini ya miaka mitano, ambapo zaidi ya watoto milioni 13 walipata usajili na vyeti vya kuzaliwa kupitia mfumo wa SMS.
“Pia tumeshirikiana na Hospitali ya CCBRT kusaidia matibabu ya watoto wenye tatizo la miguu ya kupinda (clubfoot), na tunaendelea kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya macho bure Tanzania Bara na Zanzibar ambapo tayari tumewafikia Watanzania zaidi ya 23,000,” alisema.
Rwetabura alisema Yas ipo katika mazungumzo na Taasisi ya Benjamin William Mkapa kwa lengo la kuanzisha ushirikiano wa kimkakati utakaosaidia kuendeleza miradi endelevu ya afya na maendeleo kwa wanawake, watoto na vijana.
“Yas itaendelea kuwa mshirika katika safari hii kwa kuwekeza katika suluhisho bunifu za teknolojia zitakazoimarisha mifumo yetu ya afya na kuwawezesha vijana kuleta mageuzi katika utoaji wa huduma za afya. Kwa pamoja tunaweza kujenga Tanzania yenye afya bora zaidi, iliyounganishwa zaidi na yenye ustahimilivu zaidi,” aliema Rwetabura.

More Stories
Osha yatajwa miongoni mwa Taasisi za Kimkakati nchini
Umoja wenye Malengo kukabili changamoto zinazoibuka SADC
ORCI yamjukia hali Balozi wa Saratani